Wapinzani watishia Senegal kutotawalika
29 Januari 2012Matangazo
Polisi mmoja aliuawa katika machafuko yaliyozuka siku ya ijumaa, baada ya waandamanaji kuanza kurusha mawe, kupindua magari na kuchoma matairi na polisi nao walifyatua mabomu ya kutoa machozi. Mapambano hayo yalitokea baada ya mahakama kuu nchini humo kusema Rais Wade ana haki ya kuwania tena wadhifa wake kwa awamu ya tatu.
Katika hatua nyingine hapo jana polisi, ilimkamata Alioune Tine alie kiongozi wa kundi la wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo liitwalo M23, kufuatia vurugu za ijumaa.