1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani Uganda wapania kuandamana leo

10 Mei 2011

Nchini Uganda wanasiasa wa upinzani wanajiandaa kufanya mkutano wa hadhara katikati ya mji wa kampala baadaye alasiri.

https://p.dw.com/p/11Cvq
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dr. Kiiza BesigyePicha: AP

Ifahamike kuwa polisi wamewakataza wanasiasa hao kukusanyika kwenye uwanja wa Constitution ulio na umuhimu mkubwa kisiasa. Wapinzani hao wamekuwa wakihangaishwa na polisi kila wanapojaribu kuandamana kupinga ongezeko la bei za vyakula na mafuta pamoja na kudai demokrasia. Jee hali iko vipi mjini Kampala kabla ya mkutano huo wa hadhara kufanyika? Hilo ndilo suali Thelma Mwadzaya alilomuuliza Mwandishi wetu wa Kampala Leyla Ndinda aliyekuwa katikati ya mji muda mfupi uliopita