1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapigakura wachache wateremka vituoni Cote d´Ivoire

Martin,Prema/ZPR12 Desemba 2011

Uchaguzi wa bunge umefanyika Cote dÍvoire hapo jana, lakini idadi ndogo tu ya wapiga kura walijitokeza vituoni.

https://p.dw.com/p/13QuG
Der neue Präsident der Elfenbeinküste, Alassane Ouattara, aufgenommen am 28.05.2011 nach einem Gespräch mit Frankreichs Regierungschef Fillon in Paris. Foto:Silver Gerard/Maxppp dpa
Rais Alassane Ouattara wa Cote d´IvoirePicha: picture alliance / dpa

Kiasi ya watu milioni 5.7 waliandikishwa kupiga kura katika uchaguzi huo wa bunge wa kwanza kufanyika nchini humo, tangu mwaka 2000. Chama cha rais wa sasa Alassane Ouattara, kinatazamiwa kushinda kwa wingi mkubwa, kwani chama cha rais wa zamani Laurent Gbagbo kimeususia uchaguzi huo. Ni mwaka mmoja tu tangu kumalizika kwa uchaguzi wa rais nchini humo.
Uchaguzi huo, ulisababisha machafuko na umwagaji mkubwa wa damu miongoni mwa wafuasi wa Ouattara na wa Gbagbo. Matokeo ya uchaguzi wa jana yanatazamiwa kutangazwa baadae wiki hii. Gbagbo sasa amepelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague, Uholanzi, akikabiliwa na mashtaka ya kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa machafuko kufuatia uchaguzi wa rais.