1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Wanne wauawa, Carter Center washuku matokeo ya uchaguzi

Polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema kwamba watu wanne wameuawa hapo jana katika vurugu za baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi. Milio ya risasi imesikika kutoka mji mkuu Kinshasa na jimbo la Kasai.

Machafuko ya baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa DRC.

Machafuko ya baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa DRC.

Mjini Kinshasa polisi waliripotiwa kuwazingira vijana waliokuwa wakipinga matokeo hayo. Watu kadhaa pia wamekamatwa.

Wakati huo huo, kituo cha waangalizi wa uchaguzi cha Marekani, Carter Center, kimesema idadi ya waliojitokeza kupiga kura katika ngome za rais wa sasa, Joseph Kabila, ilikuwa kubwa mno, huku kura kadhaa zikiwa hazikuhesabiwa katika ngome za mgombea wa upinzani, Etienne Tshisekedi. Kituo hicho kimesema kuwa ukiukwaji wa taratibu ambao haukufafanuliwa ulisababisha kutozingatiwa matokeo ya karibuni vituo 2000.

Ijumaa iliyopita, Tume ya Uchaguzi ilitangaza ushindi wa asilimia 49 wa Rais Kabila, huku Tshisekedi akipata asilimia 32. Bado kuna fursa ya kukata rufaani katika mahakama kuu. Ijumaa iliyopita Tshisekedi alitoa mwito pawepo utulivu.

DW inapendekeza

 • Tarehe 11.12.2011
 • Mwandishi Mohammed Khelef/ZPR
 • Mada Zinazohusiana DRC, Joseph Kabila
 • Maneno muhimu DRC
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13QiS
 • Tarehe 11.12.2011
 • Mwandishi Mohammed Khelef/ZPR
 • Mada Zinazohusiana DRC, Joseph Kabila
 • Maneno muhimu DRC
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13QiS

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com