1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Wanigeria waandamana kupinga matokeo ya uchaguzi

7 Machi 2023

Maelfu ya wafuasi wa upinzani nchini Nigeria wameandamana wakipinga matokeo ya uchaguzi uliokwisha, wakati ambapo miito ya kuandaliwa upya uchaguzi ikiongezeka.

https://p.dw.com/p/4OKs0
Nigeria Protest NLC Abuja
Picha: Uwais/DW

Wakiwa wamevalia mavazi meusi na kubeba mabango, waandamanaji hao wakiongozwa na mgombea wa chama cha People's Democratic Party aliyekuwa wa pili Atiku Abubakar, waliandamana hadi kwenye ofisi za tume ya uchaguzi nchini humo.

Walilizuia lango la kuingia katika afisi hizo huku wakitaka mamlaka ziandae uchaguzi mpya katika mazingira mazuri yatakayoleta matokeo sahihi.

Karibu vyama vitano vya upinzani nchini humo vinayapinga matokeo ya uchaguzi vikidai kulikuwa na uchakachuaji wa matokeo.

Ili kuchaguliwa kuwa rais wa Nigeria, mgombea anapaswa kupata angalau asilimia 25 ya kura katika angalau theluthi mbili ya majimbo 36 ikiwa ni pamoja na mji mkuu Abuja.