Wanasiasa waliokamatwa nchini Kenya waachiwa kwa dhamana
16 Juni 2010Naibu waziri wa barabara Wilfred Machage, Fred Kapondi mbunge wa Mt Elgon, Joshua Kutuny wa Charanganyi na mwanaharakati Christine Nyagitha. Hali mnamo siku za karibuni imekuwa tete kukiwa na mvutano kati ya makundi mawili hata miongoni mwa wanasiasa, kati ya wanaoipinga rasimu ya katiba mpya na wanaoiunga mkono.
Kupata zaidi juu ya hali ilivyo nimezungumza na Afisa wa Tume ya haki za binaadamu nchini Kenya Bw Hassan Omar Hassan, na kwanza nilimuuliza nini hasa la msingi lililotajwa kuwa ndiyo sababu ya kuwatia nguvuni wabunge hao.
Wabunge hao watatu na mwanaharakati Christine Nyagitha wote wameachiwa kwa dhamana leo baada ya kufikishwa mahakamani ambapo walikana mashtaka dhidi yao.
Hassan Omar (Kenya Human rights Commssion)
Mpitiaji:Josephat Charo