1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasiasa Afrika mbioni kuikwamua Côte d'Ivoire

Oumilkher Hamidou7 Januari 2011

Alassane Ouattara anasema yuko tayari kutoa msamaha kwa Laurent Gbagbo na kuhakikisha cheo chake kama rais wa zamani kinaheshimiwa, ikiwa naye Gbagbo ataondoka madarakani na kumkambidhi Ouattara ofisi kwa hiari yake.

https://p.dw.com/p/zuel
Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinailinda Hoteli Golf-makao makuu ya serikali ya Alassane Ouattara mjini AbujaPicha: dapd

Juhudi zimeshika kasi kuhakikisha jinsi ya kumtanahabisha rais wa Cote d'Ivoire aliemaliza wadhifa wake, Laurent Gbagbo, akubali kuyapa kisogo madaraka. Uingereza na Canada hazijajibu mwito wa Gbagbo aliyewataka mabalozi wa nchi hizo warejee nyumbani.

Nigeria na Afrika kusini wamekuwa na mazungumzo mjini Lagos kuhusu mgogoro wa Côte d'Ivoire na kutathmini mbinu za aina mpya kumtanabahisha Laurent Gbagbo ang'oke madarakani.

Mazungumzo hayo yamewaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane, na mwenzake wa Nigeria, Odein Ajumogobia.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Nigeria hakutaka kusema mengi; amedokeza tu kwamba "kila kitu kinafuata utaratibu wa kidiplomasia."

"Njia ya kijeshi haikutengwa, lakini tutafanya kila la kufanya kumtanabahisha rais Laurent Gbagbo akubali kuondoka," amesema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Nigeria.

Wakati huo huo, rais anaetambuliwa kimataifa, Alassane Outtara, amesema yuko tayari kumkubalia msamaha Laurent Gbagbo na kumpatia udhamaini na kuhakikisha cheo chake kama rais wa zamani kinaheshimiwa. Hata hivyo, Alassane Outtara anafungamanisha hayo na sharti kwamba Laurent Gbagbo anang'oka haraka madarakani."

Elfenbeinküste Sanktionen Botschafter Ausweisung
Alassane Ouattara (kulia) anamuamkia balozi wa Canada bibi Isabelle Massip(kushoto) pamoja na mabalozi wengine,katika Hoteli Golf mjini AbidjanPicha: dapd

Katika mahojiano pamoja na gazeti la Ufaransa,Le Figaro,

Alassane Outtara amemtuhumu Laurent Gbagbo kuwa na "damu mikononi mwake". Outtara amesema.

"Raia wengi wa Côte d'Ivoire wameuwawa na maajenti kutoka nje pamoja na waasi.Watu wameshauwawa,wanawake wamebakwa na maelefu wamejeruhiwa na mamluki walioletwa kutoka Liberia."

Umoja wa Mataifa. unaomtambua Ouattara kuwa ndie mshindi wa uchaguzi wa marudi wa Novemba 28, unasema watu 210 wameuwawa katika mashambulio yaliyofuatia duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa rais.

Katika mvutano wake na jumuia ya kimataifa, Laurent Gbagbo amewataka mabalozi wa Uengereza, Nicholas James Westcott, na Marie-Isabelle Maassip wa Canada waihame nchi hiyo.

Canada imelikataa onyo hilo, ikisema haikupokea amri yoyote kutoka serikali ya Alassane Outtara. Uengereza pia imesema haitambui amri yoyote isipokua ile ya serikali ya Alassane Outtara.

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/AFP, Reuters

Mpitiaji: Miraji Othman