1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waendelea kuondoka Mali

Amina Mjahid
22 Oktoba 2023

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameondoka katika kambi yao ya Tessalit iliyoko Kidal nchini Mali kama sehemu ya mpango wa kuondoka nchini humo.

https://p.dw.com/p/4XrxS
Sehemu ya kikosi cha Ujerumani kwenye ujumbe wa MINUSMA ambacho kimeondoka nchini Mali.
Sehemu ya kikosi cha Ujerumani kwenye ujumbe wa MINUSMA ambacho kimeondoka nchini Mali.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kuondoka siku ya Jumamosi (Oktoba 21) kwa Kikosi hicho cha amani cha Umoja wa Mataifa kinachofahamika kama MINUSMA, kumeongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano kati ya wanajeshi wa Mali na makundi ya wanamgambo wanaotaka kulidhibiti eneo hilo. 

Soma zaidi: Walinda amani wa umoja wa Mataifa waondoka Mali

Taarifa ya kuondoka kwa wanajeshi hao ilithibitishwa na jeshi la Chad ndani ya kikosi hicho.

Kuondoka kwa wanajeshi 11,600 na maafisa  wa polisi 1,500 wa MINUSMA kunatarajiwa kukamilika Desemba 31.