1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 32 wafungwa maisha kwa jaribio la mapinduzi Uturuk

Saleh Mwanamilongo
7 Aprili 2021

Mahakama ya Uturuki imewahukumu wanajeshi 32 wa zamani kifungo cha maisha jela kwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi lililoshindwa la mwaka 2016.

https://p.dw.com/p/3rgto
Türkei Putschversuch Gefängnis in Sincan
Picha: Burhan Ozbilici/AP/picture alliance

Wanajeshi hao ni miongoni mwa wanajeshi wazamani 497 wakiwemo wa kikosi cha ulinzi wa rais.Hukumu hiyo imesomwa katika chumba kikubwa kabisa cha mahakama iliyojengwa mahususi kusikiliza kesi za jaribio hilo la mapinduzi katika gereza la Sincan mjini Ankara.

''Wanaotaka mapinduzi watathmini vyema kesi hii''

Shirika la habari la taifa, Anadolu mwanzo lilitangaza hukumu ya kifungo cha maisha kwa maafisa wanne, lakini wakili wa Ikulu ya rais Erdogan aliliambia shirika la habari ya AFP kwamba  ni wanajeshi wazamani 22 waliohukumiwa kifungo cha maisha jela. Alaadin Varol, wakili wa serikali ya Uturuki amesema kuwa hukumu hiyo ni funzo kwa wanaotaka mapinduzi.

''Maafisa wote walihosika katika jaribio la mapinduzi wamehukumiwa kifungo cha maisha jela. Nimetaka kuwaambia wengine wanaotaka mapinduzi watathmini vyema kesi hii. Ni hukumu ya juu kabisa nchini mwetu ambayo wamepewa leo , nchi yetu ingekuwa na adhabu ya kifo kama wamehukumiwa pia kifo.''

 Washukiwa walikutwa na hatia kadhaa,ikiwemo jaribio la kuipindua serikali halali kikatiba. Mahakama iliwakuta pia na hatia ya kufanya mashambulizi dhidi ya kituo cha televisheni ya taifa TRT na kuwalazimisha waandishi habari kusoma ujumbe wa wanamapinduzi na vilevile shambulizi dhidi ya ngome ya jeshi.

Maafisa wa polisi wa Uturuki wakipiga doria nje ya mahakama ya uhalifu mjini Ankara.
Maafisa wa polisi wa Uturuki wakipiga doria nje ya mahakama ya uhalifu mjini Ankara.Picha: Stringer/AFP

 Novemba, watu 337,wakiwemo maafisa na marubani,walihukumiwa kifungo cha maisha jela, kufuatia kesi maalumu ya jaribio hilo la mapinduzi ya Julai 15, mwaka 2016.

Kamatakamata bado yaendelea 

 Kesi dhidi ya kikosi hicho ilianza kusikilizwa mnamo mwezi Oktoba mwaka 2017. Jaribio la mapinduzi lilisababisha vifo vya watu 251 na wengine zaidi ya 2000 kujeruhiwa, mbali na waliohusika na jaribio la mapinduzi waliouliwa usiku wa tukio. Uturuki inamtuhumu Fethullah Gulen,mshirika wa zamani wa rais Erdogan, kwa kupanga jaribio hilo la mapinduzi, madai ambayo anayakanusha.

Usiku wa kuamkia tarehe 16 Julai mwaka 2016,mji wa Ankara ulishuhudia machafuko kufuatia kundi la wanajeshi waliojaribu kuipindua serikali ya rais Recep Tayip Erdogan. Ndege za kivita za Aina na F16 yiliyalenga makao makuu ya bunge, makao makuu ya polisi ,kikosi cha ulinzi wa rais  na barabara zinazoelekea Ikulu. Mashambulizi hao ya anga yalisababisha vifo vya watu 68 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa kwenye mji mkuu Ankara.