1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 27 wauwawa nchini Syria

15 Desemba 2011

Waasi kutoka katika jeshi la Syria leo hii wameripotiwa kuwauwa wanajeshi 27 wa serikali, huku makundi ya haki za binadamu nchini humo, yakitaja majina ya maafisa 74 wanaodaiwa kuamuru kushambilia kwa waandamanaji.

https://p.dw.com/p/13TL2
This image from amateur video made available by the Ugarit News group on Monday, Dec. 12, 2011, purports to show security forces in Daraa, Syria. (Foto:Ugarit News Group via APTN/AP/dapd) THE ASSOCIATED PRESS CANNOT INDEPENDENTLY VERIFY THE CONTENT, DATE, LOCATION OR AUTHENTICITY OF THIS MATERIAL. TV OUT
Mapigano katika mji wa DeraaPicha: dapd

Kwa mujibu wa makundi hayo ya haki za binadamu, mapigano hayo ni miongoni mwa mashambulio makubwa kabisa kutokea kufanywa na kundi la waasi tangu kuanza kwa vuguvugu la kuipinga serikali ya Syria miezi minane iliyopita.

Vita hiyo ilitokea huko jimbo lililokusini mwa nchi hiyo la Deraa ambapo kumetajwa kuongezeka kwa mapigano ambayo yanelekea kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Likimnukuuu shuhuda mmoja, Shirika la Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake makuu mjini London limesema matukio matatu tofouti ya mapigano makali yalizuka katika maeneo ya jimbo hilo.

Mpaka sasa hakuna yeyote aliejitangaza kuhusika na mauwaji hayo lakini kundi la wanajeshi waasi kutoka katika jeshi la Syria, ambalo limejikita sana huko Uturuki, katika siku za nyuma limekuwa likifanya mashambulizi yanayofanana na hayo.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 5,000 wameuwawa tangu kuanza kwa maandamano ya kupinga serikali ya nchi hiyo miezi minane iliyopita. Jambo hilo limeutia utawala wa rais Bashar al Assad katika mlolongo kuimbwa wa vikwazo pamoja na kutengwa na jumuiya ya kimataifa.

Außenminister Guido Westerwelle (FDP) begruesst am Montag (12.12.11) in New York (USA) die Hohe Kommissarin der Vereinten Nationen fuer Menschenrechte (UNHCHR), Navi Pillay. Die Zahl der Todesopfer bei den Protesten in Syrien ist deutlich gestiegen. "Wir muessen davon ausgehen, dass etwa 5.000 Menschen bereits ihr Leben gelassen haben", sagte Aussenminister Guido Westerwelle am Montag nach dem Treffen mit Pillay in New York. Bislang hatten die Vereinten Nationen die Zahl der Todesopfer auf 4.000 geschaetzt. (zu dapd-Text) Foto: Oliver Lang/dapd
Navi Pillay na Guido Westerwelle mjni New YorkPicha: dapd

Tayari Marekani imekwisha tabiri kuanguka kwa utawala wa Syria kufuatia vitendo vyake kwa umma wa nchi hiyo.

Afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, Frederic Hof aliliambia bunge la nchi hiyo kwamba, ni kweli kwamba ukandamizaji wa Assad utamfanya awepo madarakani lakini ni kwa muda mfupi.

Afisa huyo alisogea mbele kidogo kwa kusema utawala huo ni sawa na mfu anaetembea.

Nalo, Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema limewatambua maafisa 74 wa serikali ya Syria ambao wanadai kuwa wanawajibika moja kwa moja na kuwashambulia waandamanaji wasio na silaha katika vuguvugu la miezi minane lenye shabaha ya kuipinga serikali ya rais Assad.

Maafisa hao ni pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Syria, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Usalama wa Taifa pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Anga. Kundi hilo la haki za binadamu lenye makao yake makuu mjini NewYork, nchini Marekani limewatuhumu maafisa hao wa ngazi za juu kwa kuamuru kufanyika maouvu kwa waandamanaji.

Tuhuma jumla zilizoanishwa na Human Rights Watch ni kuamuru mauwaji yaliyofanyika katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, mateso, na kuwatia watu kizuizini kinyume cha sheria.

Kutoka na hali hiyo Shirika hilo la haki za binadamu limetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwasilisha juu ya hali ya mambo kwa mahaka ya uhalifu ICC na kuweka vikwazo kwa maafisa wanahusishwa na uovu huo.

Mwandishi: Sudi Mnette//DPA//APE
Mhariri:Abdul-Rahman