1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wataka miito yao kulinda bayoanuwai isikizwe

8 Desemba 2022

Maandamano, mijadala ya umma na maonesho ya filamu ni baadhi ya yanayoshuhudiwa katika mkutano wa COP15 ambapo mashirika yanahamasisha kuhusu haja ya kulinda bayoanuwai.

https://p.dw.com/p/4Kg5q
UN-Artenschutzkonferenz COP 15 in Montreal, Kanada 2022 | Indigene Protestierende
Picha: Andrej Ivanov/AFP/Getty Images

Katika azma yao kupaza sauti ili miito yao isikizwe, zaidi ya mashirika 100 hivi karibuni yaliungana kuunda kile ambacho kinaitwa "COP15 Pamoja" wakilenga mkutano wa kilele wa utunzaji wa bayoanuwai ulioanza Disemba 7 na utamalizika Disemba 19 mjini Montreal nchini Canada.

Msemaji wa kundi hilo la mashirika Anne-Celine Guyon aliliambia shirika la habari la AFP kwamba si swali tu tena la watetezi wa mazingira. Kila mmoja yuko mezani, kila mmoja anataka kufanya jambo na ni hali inayotia moyo. aliongeza kuwa nyakati hizi ni za kihistoria kwa jimbo la Quebec, Canada kunakofanyika mkutano huo.

Wanaharakati hao wameshikilia kuwa sharti wasikizwe ndani ya ukumbi ambako wajumbe wanashauriana na kujadiliana, na vilevile wasikizwe mitaani kupitia maandamano yao.

Mkutano mrefu wa mazingira wa UN wamalizika bila makubaliano

Warsha na mijadala ya wazi kujadili utunzaji bayoanuwao

Mijadala hiyo ni wazi kwa yeyote kushiriki lakini pia kuna warsha kadhaa ambazo zimeandaliwa.

Tukio kubwa zaidi litakuwa kile wamekiita "Maandamano mazuri kwa walio hai" Disemba 10. Wanaoyapanga maandamano hayo wanatarajia maelfu ya watu kushiriki.
Tukio kubwa zaidi ya wanaharakati pembezoni mwa mkutano wa Montreal litakuwa kile wamekiita "Maandamano mazuri kwa walio hai" Disemba 10. Wanaoyapanga maandamano hayo wanatarajia maelfu ya watu kushiriki.Picha: Anna Kurth/AFP/Getty Images

Albert Lalonde, mwenye umri wa miaka 20 ambaye pia ni meneja wa mradi unaosimamiwa na Wakfu wa David Suzuki, amesema baada ya janga la Covid kuvuruga mambo katika miaka miwili iliyopita, mkutano wa COP15 utakuwa muhimu kwa wadau husika kukutana tena na kufufua nahusiano.

 Japo hakuna viongozi wa serikali wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo isipokuwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeu, waandalizi wanatumai mkutano wa kilele wa COP15 utafikia msukumo wa klisiasa sawa na makubaliano ya Paris. Amesema Eddy Perez ambaye pia ni msemaji wa kundi hilo.

COP15: Bioanuwai ni nini na kwa nini ni muhimu sana?

Utafiti wa maoni uliofanywa ya shirika la Greenpeace hivi karibuni nchini Canada ulionesha watu wanane kati ya kumi wanaamini serikali inapaswa kuongoza kwa kuweka ahadi thabiti za kulinda mazingira, hivyo kuwa mfano mzuri.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akifungua mkutano wa utunzaji bayoanuwai mjini Montreal.
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akifungua mkutano wa utunzaji bayoanuwai mjini Montreal.Picha: Christina Muschi/REUTERS

"Watu wanaanza kuelewa kwamba tuko katika hali hatari. Kwamba kuna maelfu ya aina mbaimbali ya viumbe vilivyoko hatarini katika sayari yetu," ndivyo anavyoamini Marie-Josee Beliveau wa shirika la Greenpeace tawi la Canada.

Miito yaongezeka ya kutunza bayoanuwai

Akiwa na matumaini makubwa kwamba mkutano huo utakuwa wenye tija, amesema wajumbe wanapaswa kujua wanaharakati waliojitolea kisawasawa wanafuatilia mijadala yao kwa karibu.

Anne-Sophie Dore, wakili wa masuala ya mazingira na pia mhadhiri amesema, kuna mwamko kuhusu masuala ya ulinzi wa bayoanuwai labda zaidi ya hapo nyuma.

Wadudu walio hatarini kutoweka

Kwingineko, jamii asilia ya Canada imetaka kwamba kwa bayoanuwai yapaswa kupewa kipaumbele zaidi.

Kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, ardhi ya jadi ya jamii hiyo ni nyumbani kwa asilimia 80 ya bayoanuwai ambayo imesalia duniani.

(AFPE)

TAfsiri: John Juma

Mhariri: Zainab Aziz