1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki sawaUganda

Wanaharakati Uganda waikosoa EU kufuatia sheria ya LGBTQ

8 Septemba 2023

Wanaharakati wa kutetea haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wamekosoa tangazo la Umoja wa Ulaya wiki hii kwamba hautaifutia ufadhili kwa Uganda kuhusiana na sheria yake kali dhidi ya mashoga.

https://p.dw.com/p/4W7vq
Uganda Anti LGBTQ Bill
Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Kwenye taarifa iliyowasilishwa katika bunge la Ulaya siku ya Jumatano, kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ulaya Jutta Urpilainen alisema kuondoa msaada wa kifedha kwa Uganda kutawanyima watu walio katika mazingira magumu msaada muhimu.

Wanaharakati wa haki za binadamu wa Muungano ujulikanao kama Convening for Equality (CFE) walisema kupitia taarifa kwamba msimamo wa Umoja wa Ulaya umeshindwa kuhakikisha fedha zake hazitasaidia dhuluma na ubagudi dhidi ya  jamii ya LGBTQ.

Sheria iliyopitishwa dhidi ya vitendo vya ushoga nchini Uganda inatoa adhabu kali ikiwemo uwezekano wa hukumu ya kifo kwa washukiwa.