CHICAGO:
Watu 5 wameuawa na 18 wamejeruhiwa katika ufyatuaji wa risasi uliotokea katika Chuo Kikuu kimoja karibu na mji wa Chicago nchini Marekani.Miongoni mwa waliofariki ni mshambuliaji aliejipiga risasi mwenyewe.Inasemekana kuwa kijana huyo mzungu alikuwa na bastola na bunduki inayopiga risasi kwa mfululizo na aliwalenga wanafunzi katika ukumbi wa mihadhara katika Chuo Kikuu cha Illinois ya Kaskazini.Watu wengi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu hospitalini.Baadhi yao wana majeraha mabaya vichwani.