Wakili akosoa hatua ya polisi kuhusu sakata la viongozi wa gazeti la Standard nchini Kenya
17 Aprili 2007Matangazo
Kwa mujibu wa habari hizo, Artur Magarian alidai kwamba alitakiwa na waziri mmoja wa ngazi ya juu kuchunguza akaunti za mbunge Gideon Moi, mtoto wa Rais wa zamani Daniel Arap Moi huko Dubai na kuandaa mpango wa kumteka nyara. Gazeti hilo liliwasilisha polisi kanda za mahojiano hayo kama ushahidi. Je hatua ya polisi kuwatia nguvuni na kutaka viongozi wa gazeti hilo watoe ushahidi ilikuwa ni ya halali?
Mohamed Abdulrahman alizungumza na mwanasheria Harun Ndubi kwa njia ya simu akiwa mjini Nairobi ambaye kwanza alikuwa na haya ya kueleza.