1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa nyuklia wa Iran wafikiwa

14 Julai 2015

Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani wamefikia makubaliano muhimu leo mjini Vienna , kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kuweza kuondolewa vikwazo ilivyoekewa na mataifa ya magharibi

https://p.dw.com/p/1FyFd
Österreich Atomverhandlungen mit dem Iran in Wien
Picha: Reuters/C. Barria

Wakati huo huo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameyaeleza makubalino hayo ni kosa kubwa la kihistoria na kusema atafanya kila kinachowezekana kuzuwia nia ya Iran ya kujipatia silaha za kinyuklia.

Makubaliano hayo yamekuja katika siku ya 18 za mbio katika mazungumzo kati ya Iran na kile kinachojulikana kama kundi la P5 +1, mataifa matano ambayo ni Marekani , Urussi , China , Uingereza, Ufaransa pamoja na Ujerumani , mjini Vienna.

"Makubaliano yamekamilika," mwanadiplomasia mmoja ameliambia shirika la habari la AFP katika mji mkuu wa Austria , Vienna , mahali ambapo mkutano wa mwisho wa mawaziri kati ya Iran na mataifa makubwa uliitishwa.

Wien Atomgespräche Iran
Rais wa Iran Hassan Rouhani asema mkataba huo ni ukarasa mpyaPicha: Getty Images/AFP/J. Klamar

Makubaliano yanatarajiwa kuzuwia kwa kiasi kikubwa mpango wa kinyuklia wa Iran na kuweka ukaguzi mkali wa Umoja wa mataifa ili kuwezesha kuzuwia kabisa utengenezaji wa silaha za kinyuklia na kufanya kuwa rahisi kugundua hatua kama hizo.

Kwa upande wake , vikwazo vya mataifa ya magharibi vinavyoikaba Iran katika uuzaji wa mafuta na uchumi wa nchi hiyo yenye wakaazi milioni 78 vitaondolewa kwa taratibu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif ameyasifu makubaliano ya kinyuklia kuwa ni "suluhisho la kila upande kushinda". Ameongeza kwamba makubaliano hayo yanafungua upeo mpya kwa ajili ya kukabiliana na matatizo magumu zaidi ya dunia.

Waziri mkuu wa Israel amesema atafanya kila linalowezekana kuzuwia nia ya Iran kujipatia silaha za kinyuklia.

"Iran itapata njia ya uhakika kuelekea kupata silaha za kinyuklia, amesema Netanyahu. Vikwazo vingi ambayo vimekusudiwa kuizuwia Iran kujipatia silaha hizo vitaondolewa," Netanyahu amesema mwanzoni mwa mkutano na waziri wa mambo ya kigeni wa Uholanzi Bert Koenders mjini Jerusalem.

Iran itajipatia fedha nyingi, mabilioni ya dola , ambazo zitaiwezesha kuendelea na mabavu yake na ugaidi katika eneo hili na duniani. Haya ni makosa mabaya kabisa bila kiasi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na waziri mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif wamekuwa muhimu katika kumaliza mzozo huu kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe

Mhariri: Mohammed Abdul- Rahman