1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waislamu wenye itikadi kali Ujerumani

Julia Bernstorf1 Desemba 2015

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama, Ujerumani wanaishi maelfu ya waislamu wenye itikadi kali. Watu hao wamegawanyika katika makundi tofauti na wana malengo tofauti. Haya ni baadhi ya makundi na viongozi.

https://p.dw.com/p/1HCUS
Waislamu wenye itikadi kali
Picha: picture-alliance/dpa/B. Roessler

Kwa mujibu wa shirika la upelelezi wa uhalifu nchini Ujerumani, vijana wanazidi kujiunga na makundi ya wanajihadi na kufumba na kufumbua wanakuwa tayari wanafuata itikadi kali. Baadhi ya wakati panapita wiki tu au miezi hadi hadi mtu huyo anapoelekea Syria, amesema mwenyekiti wa shirika la upelelezi Holger Münch katika maohojiano pamoja na gazeti la "Die Welt." Kiasi cha wafuasi wa itikadi kali 750 wasiochelea kutumia nguvu wameondoka Ujerumani mpaka sasa na kuelekea Syria. Thuluithi moja kati yao wamesharejea nchini na 70 kati yao wamejipatia maarifa ya kupigana.

Mbinu za kuwasajili wapiganaji wengine wa "vita vya jihadi" zinaonyesha bado hazijesha. Mashirika ya upelelezi wa ndani na nje ikiwa ni pamoja na shirika la BKA wanakadiria,wakati huu tulio nao wafusi 43.000 wa itikadi kali wanaishi nchini Ujerumani. Hao ni watu wanaotaka kuigeuza dini ya Kiislamu iwe mwongozo wa maisha yao.Idadi ya wasalafi imeendelea kuongezeka miaka ya nyuma. Maafisa wa idara za usalama wanakadiria watu wasiopungua 7900 wamo katika kundi hilo. Wasalafi wanafuata tafsiri ya sheria ya dini ya Kiislamu kama ilivyotajwa katika Quran na maagizo mengine ya dini ya Kiislamu. Si wasalafi wote walioko tayari kutumia nguvu ili kutekeleza imani yao. Hata hivyo kwa mujibu wa kiongozi wa shirika la upelelezi la BKA Holger Münch idadi yao inazidi kuongezeka.Hali hiyo shupavu inapaliliwa na makundi tofauti pamoja na mashekhe wenye kutoa hotuba kali kali.

Mashekhe pamoja na makundi yafuatayo ya kidini walioorodheshwa kwa mpangilio,wanatajikana kuwa na ushawishi mkubwa katika uwanja wa wafuasi wa itikadi kali ya dini ya Kiislamu nchini Ujerumani.

Wanawake Wajerumani wakipigana sambamba na Dola la Kiislamu
Wanawake Wajerumani wakipigana sambamba na Dola la KiislamuPicha: picture-alliance/dpa

Ansarul Aseer

Ansarul Aserr, ikimaanisha "msaidizi wa wafungwa" ni kundi la wasalafi wanaowashughulikia zaidi waislam waliofungwa jela. Wengi wao wanatokea katika makundi ya jihadi na ambao kutokana na kuunga mkono ugaidi, wanatumikia kifungo jela hapa hapa nchini Ujerumani au nchi za nje. Shirika hilo linasajili wafuasi wepya miongoni mwa wafungwa. Ansarul Aseer linautumia ukurasa wake wa mtandao kuwataka watu wawe na maingiliano na wafungwa na kuwasaidia kiroho.Mtandao huo unazungumzia kuhusu waliofunguliwa kutoka jela, kesi na hukmu zinazotolewa.

Daesh - Dola la Kiislamuu

Propaganda za lile kundi linalojiita "Dola la Kiislamuu", kwa kiarabu "Daesh" zimeingia mpaka Ujerumani, kupitia mtandao.Kundi hilo la kigaidi lililopigwa marufuku linadhibiti sehemu kubwa ya ardhi ya Syria na Iraq. Mwaka 2014, kiongozi wake, Abu Bakr al-Baghdadi, alitoa wito wa kuundwa utawala wa wasunni wanaofuata mwongozo wa dini ya Kiislamu - Khalifa. Wapiganaji zaidi ya elfu kumi wamejiunga na kundi hilo la wanajihadi - miongoni mwao wakiwemo mamia kadhaa kutoka Ujerumani.

Mwanamuziki wa Rap wa zamani kutoka Berlin, Denis Cuspert, maarufu kwa jina la Deso Dogg, amejiunga na kundi hilo pengine tangu mwaka 2012.Katika kanda moja ya video ya IS, anatoa wito wa kufanywa mashambulio nchini Ujerumani na kuonekana - katika kanda nyengine ya video inayoonyesha jinsi walivyokuwa wakiwakata watu vichwa, jinsi alivyogeuka kuwa mweneza propaganda mkubwa wa Daesh anaezungumza kijerumani. Oktoba mwaka 2015 inasemekana ameuwawa kufuatia hujuma za mabomu ya kimarekani. Mpaka leo bado wafuasi wa itikadi kali ya din i ya Kiislamu wanasafiri kutoka Ujerumani kuelekea Syria na Iraq, kupigana upande wa IS.

Gemeinde des Imams Hassan Dabbagh
Msikiti wa Imam Hassan DabbaghPicha: picture-alliance/dpa/W. Grubitzsch

Hassan Dabbagh

Hassan Dabbagh ni Mjerumani mwenye asili ya Syria na anatajikana kuwa miongoni mwa viongozi muhimu wa itikadi ya salafi nchini Ujerumani. Anawatenganisha watu kwa makundi ya "waislam" na "wasioamini dini". Dabbaagh ni mwenyekiti wa shirika na apia Imam wa msikiti wa Al Rahman mjini Leipzig ambako kila mara anakuwa akiandaa warsha na majadiliano kuhusu dini ya Kiislamuu. Katika ripoti ya idara ya upelelezi ya jimbo la Sachsen iliyochapishwa 2014, imetajwa kwamba mawaidha yake makali yanatosha kuwashawishi tangu vijana ,mpaka waislam wasiojiamini pamoja pia na watu waliosilim wafuate itikadi kali.Zaidi ya hayo Dabbagh ameanzisha utaratibu wa kueneza taluma ya dini ya Kiislamu kwa kuyatembelea maeneo tofauti humu nchini.Mawaidha yake pia yamejaa mtandaoni.

Msaada kwa wasiojimudu

Shirika la Msaada kwa wasiojimudu limeundwa mjini Neuss mwaka 2013. Linaangaliwa kama shirika linalowasaidia waislam wanaotaabika.Wizara ya mambo ya ndani ya jimbo la North Rhine- Westphalia (NRW) linahisi hata hivyo kuna mambo yanayoonyesha shirika hilo si chochote chengine isipokuwa vuguvugu la itikadi kali la salafi. "Katika hafla iliyoandaliwa na shirika hilo kwaajili ya kukusanya misaada,shirika la upelelezi la NRW linasema walijitokeza mara nyingi mashekhe ambao wanajilikana kuhusika na itikadi kali za salafi.

Ibrahim Abou-Nagie

Ibrahim Abou-Nagie amezaliwa mwaka 1964 katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katika ukanda wa Gaza. Mwaka 1994 alipata uraia wa Ujerumani.Hata bila ya kupata mafunzo ya theolojia, Abou-Nagie, anaangaliwa kuwa mhutubu wa salafi mwenye ushawishi mkubwa kabisa nchini Ujerumani. Nyaraka zake ambamo anapigania tafsiri ya Qoran kama ilivyo, amezieneza katika mtandao. Anawatenganisha moja kwa moja wale anaowaita "waislamu na makafiri" - watu wasiokuwa na dini."

Abou-Nagie anasimamia tovuti aliyoipa jina "Dini ya kweli". Wanaachama wa mtandao wenye jina hilo hilo wanaeneza kampeni ya "Soma" - wanagawa misahafu katika miji ya ujerumani. Katika ripoti ya shirika la upelelezi ya mwaka 2014 imetajwa kwamba kuna ushahidi wa waatu ambao kwanza wanagawa misahafu ili baadae kushiriki katika mapigano nchini Syria.

Waislamu wenye itikadi kali wakigawa Quarn bure kwa wapitanjia.
Waislamu wenye itikadi kali wakigawa Quarn bure kwa wapitanjia.Picha: picture-alliance/dpa/J. Stratenschulte

Jumuiya ya Kiislamuu ya Milli Görus -(IGMG)

Jumuia ya Kiislamuu ya Milli Görus (kwa kiswahili"Mtazamo wa kitaifa)-kwa kifupi IGMG - linaangaliwa kuwa jumuia kubwa kabisa ya waislam nchini Ujerumani. Milli Görus ina wanachama 31.000 lakini idadi ya watu wanaojitambulisha nalo ni kubwa mno. Jumuiya ya IGMG limeundwa mwishoni mwa miaka ya 60 na mwanasiasa wa Uturuki Necmettin Erbakan.Wawakilishi wake wanazitaja ubepari na uzayuni kuwa ndio chanzo cha ukosefu wa haki ulimwenguni na kuwasihi wafuasi wake wasifunge urafiki na "watu wasioamini dini". Kiongozi wa IGMG,Mustafa Kamalak anautaja Umoja wa Ulaya kuwa ni "kilabu ya wakristo" na Umoja wa wenye ueneza dini ya kikristo". Katika toleo la gazeti la IGMG Milli Gazete lililochapishwa nchini Ujerumani mwezi juni mwaka 2013 iliandikwa: "Ni uzushi kutukuza sheria zilizotungwa na binaadamu badala ya zile sheria za Mungu."

Kikosi cha Lohberg

Mwaka 2013 walikuwa vijana kama 20 hivi kutoka eneo la Dinslaken katika jimbo la North Rhine Westphalia walioelekea Syria kujiunga na Jihad. Wengi wao waölitokea katika mtaa wa Lohberg na kujiita "kikosi cha Lohberg". Kundi hilo,kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari,lilimfuata yule aliyejiita "mhutubu Mustafa T. na baadae kufuata itikadi kali.

Wanajihadi wasiopungua wanne kutoka Dinslaken wameuliwa nchini Syria na angalau mmoja alijiripua katika shambulio la kuyatoa mhanga maisha. Mwanachama mmoja wa kundi hilo alikamatwa mapema mwaka huu: Nils D, alirejea Ujerumani Novemba mwaka 2014. Kesi dhidi yake itafunguliwa Januari mwakani.

Pierre Vogel akitoa matangazo Hamburg
Pierre Vogel akitoa matangazo HamburgPicha: picture-alliance/dpa

Pierre Vogel

Pierre Vogel anatajwa kuwa mmojawapo wa wafuasi wa itikadi kali wenye ushawishi mkubwa kabisa nchini Ujerumani. Mhutubu huyo aliyesilimu tangu mwaka 2006 anaendesha harakati chungu nzima. Hoja zake zinazozusha mabishano anaziieneza kupitia video mitandaoni na kuwalenga zaidi vijana. Vogel anasema ni jambo la lazima kwa mwanamke wa Kiislamu kujifunika kichwa.Pierre Vogel anahisi lakini matumizi ya nguvu dhidi ya wasiokua na hatia,mashambulio ya kigaidi na mwauwaji kwaajili ya kutakasa hadhi ya familia,hayaambatani na mwongozo wa dini ya Kiislamu.Kwa mujibu wa idara kuu inayoshughulikia masuala ya elimu nchini Ujerumani Pierre Vogel ana mtazamo mkali unaowatenganisha waislam anaowaangalia kuwa ni watu wema na wale ambao si waislam anaohisi kuwa si watu wema..Kwa maoni ya idara ya upelelezi mawaidha ya Pierre Vogel yanaweza kuwashawishi vijana wafuate itikadi kali ya dini ya Kiislamu.

Kundi la "Polisi wa Sharia" Wuppertal
Kundi la "Polisi wa Sharia" WuppertalPicha: Shariah-Polizei-Germany/Facebook

Sven Lau

Sven Lau ni rafiki mkubwa wa Pierre Vogel. Mtoto huyo wa kiume ambae wazee wake ni wakatoliki amesilimu mwaka 2000 na kubadilika miaka michache baadae na kugeuka salafi. Hadi mwaka 2008 alikuwa akifanya kazi kama mkuu wa zima moto katika mji wa Mönchengladbach.Baadae akafungua duka la vitabu na zana za KiislamuKwa muda mrefu alikuwa mwenyekiti wa jumuia iliyokuwa ikijiita "Mwaliko wa Peponi e.V."

Kuna wanaosema kwamba miaka ya nyuma Sven Lu alikwenda Syria mara kadhaa ili kutoa "misaada ya kiutu." Septemba mwaka 2014 na kupitia mitandao ya kijamii,mfano wa Facebook,Lau akazusha ghadhabu alipochanganyika na baadhi ya wasalafi mjini Wuppertal na kuunda kile walichokiita "Polisi wa sheria"-wakijaribu kuwazuwia vijana wa Kiislamu kuingia katika kumbi za kamari na mikahawa. Mwendesha mashtaka akafungua kesi dhidi yake kwa makosa ya kwenda kinyume na haki ya watu kukusanyika.

Tauhid Ujerumani ( iliyokuwa ikijulikana zamani kama Millatu Ibrahim)

"Tauhid Germany" au "Tauhid Deutschland" inaangaliwa kama jumuia iliyokamata nafasi ya ile ya Millatu Ibrahim. Jumuia zote hizo mbili zimepigwa marufuku nchini Ujerumani. Lakini zinaendelea na shughuli zao za kueneza propaganda za itikadi kali kupitia mtandao.Jumuia hiyo ina tovuti yake na inatumia sana pia mitandao ya kijamii mfano wa Facebook na YouTube. Miongoni mwa kanda za video zilizoonyeshwa na Tauhid Germany kuna ripoti zinazosifu matumizi ya nguvu.Baadhi ya ripoti zake zinahimiza chuki ya "wasioamini dini." Mwanajihadi wa kijerumani aliyeuliwa nchini Syria mwaka 2015, Denis Cuspert anatajikana kuwa kiongozi wa kundi hilo.Pamoja na wanachama wengine wa Millatu Ibrahim" amejiunga na wfuasi wa Dola la Kiislamu IS.

Kundi la Wolfsburg

Wanajihadi wasioopungua 20 waliondoka Wolfsburg mwaka 2013 na 2014 na kuelekea Iraq na Syria ili kupigana upande wa wanamgambo wa Dola la Kiislamu IS.Wanachama wawili wa kundi la Wolfsburg, Ayoub B na Ibrahim H.B. wanafikishwa mahakamani. Walikwenda Syria mwaka 2014 kwa kupitia nchini Uturuki. Ibrahim H.B. amesema mahakamani kundi lao linafuata itikadi kali baada ya kushawishiwa na hatibu wa IS Yassin O. ambae hivi sasa amekimbilia Syria." Alikuwa akijionyesha kana kwamba "ana jibu la kila suala" ameelezea mshitakiwa huyo jinsi kundi lake walivyoshaweishiwa na hatibu huyo."Wote wakimheshimu." Washitakaiwa hao wawili wanakabiliwa na kitisho cha kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 10 jela. Waafuasi wasiopungua 7 wa kundi la Wolfsburg wameuwwa nchini Syria.

Mwandishi: Allmeling,A/Knipp,K/Ricking C/Walter J

Tafsiri: Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman