1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi wazishambulia meli za Marekani kwa droni

Zainab Aziz
4 Desemba 2023

Jeshi la Marekani limesema meli zake za kivita zilizidunguwa ndege tatu zisizo na rubani ili kujilinda kwenye mashambulizi yaliyodumu kwa saa nzima siku ya Jumapili (Disemba 3).

https://p.dw.com/p/4Zknm
Meli ya kivita ya Marekani, USS Carney, ilishambuliwa siku ya Jumapili na droni za Wahouthi wa Yemen kwenye Bahari ya Sham.
Meli ya kivita ya Marekani, USS Carney, ilishambuliwa siku ya Jumapili na droni za Wahouthi wa Yemen kwenye Bahari ya Sham.Picha: U.S. Navy via AP/picture alliance

Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamethibitisha kufanya mashambulizi mawili ya makombora yaliyozilenga meli tatu za kibiashara kwenye Bahari ya Sham.

Tukio hilo linaashiria kuongezeka kwa mfululizo wa mashambulizi ya baharini katika Mashariki ya Kati yanayohusishwa na vita vya Israel na Hamas.

Soma zaidi: Meli ya kivita ya Marekani yazuia mashambulizi ya Wahouthi

Iran, ambayo inatuhumiwa kuliunga mkono kundi la waasi wa KIhouthi nchini Yemen,  mpaka sasa haijasema chochote kuhusiana na mashambulizi hayo.

Kwa upande wake, Marekani ilisema ingechukuwa hatua zote zinazohitajika kujibu mashambulizi dhidi yake.