1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri: wanaowaongoza maharamia wakamatwe

Abdu Said Mtullya19 Aprili 2012

Wahariri wa magazeti leo wanauzungumzia uamuzi wa serikali ya Ujerumani wa kuikubali sera ya Umoja wa Ulaya juu ya kupambana na maharamia kwenye pembe ya Afrika.

https://p.dw.com/p/14gwu
Wanajeshi wakiwasaka maharamia
Wanajeshi wakiwasaka maharamiaPicha: picture-alliance/dpa

Wahariri pia wanatoa maoni yao juu ya mkutano wa waislamu wa Ujerumani unaofanyika leo mjini Berlin.

Juu ya uamuzi wa serikali ya Ujerumani ambao bado unasubiri kupitishwa na bunge mwezi ujao, gazeti la "Stuttgarter"kwa mbali uamuzi huo unavutia, kwamba sasa maharamia watapigwa vita hadi katika nchi kavu.Mpaka sasa limekuwa jambo la kukatisha tamaa kwamba maharamia wameweza kutenda uhalifu na kukimbilia nchi kavu ambako walikuwa salama.Kwani harakati za kupambana nao zimekuwa zinaishia majini tu.

Hata hivyo uamuzi wa kuwafuatilia maharamia hadi nchi kavu maana yake ni kuanzisha vita vitakayvoshindikana. Nchi zinazoshiriki katika operesheni ya Atalanta hazitaweza kushinda katika vita hivyo.

Mhariri wa gazeti la "Straubinger Tagblatt" anasema ili kuwashinda maharamia inapasa kuwapiga vita wale wanaowaongoza maharamia hao. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kuwa mpaka sasa nchi za Ulaya zinakabaliana na dalili tu za tatizo la uharamia na siyo na kiini chake. Uharamia hautakwisha madhali mamilioni yanayotokana uhalifu huo yanangia katika mifuko ya wale wanaowaongoza wahalifu hao. Kwa hivyo sasa umefika wakati wa kuwasaka watu hao kwa udhabiti ule ule kama jinsi maharamia wanavyopigwa vita baharini. Mhariri wa "Reutlinger General-Anzeiger"anaiunga mkono hoja hiyo kwa kusema kwamba jambo muhimu sasa ni kukikabili kiini cha tatizo!

Gazeti la"Frankfurter Allgemeine" linauzungumzia mkutano wa waislamu  wa Ujerumani unaofanyika mjini Berlin. Anasema,madhali suala muhimu linalojadiliwa kwenye mkutano huo ni njia ya kuwaingiza waislamu katika jamii ya walio wengi nchini Ujerumani, pana haja ya kuvifananua vigezo vya mchakato wa kulitekeleza lengo hilo.

Mhariri huyo anafafanua; Jina la mkutano huo, linababaisha. Kwani mkutano huo siyo hasa wa masuala ya kidini bali ni wa masuala ya kijamii. Wajumbe hawajadili juu ya dini ya kiislamu bali wanatafakari njia za kuwaingiza katika jamii ya walio wengi, waislamu wanaoishi nchini Ujerumani. Kwa hivyo kinachohitajika ni kuweka utaratibu wa kufaa ili kuweza  kulitekeleza lengo hilo. Na jambo la msingi siyo mrengo wa kidini bali jinsi kila mwislamu anavyohusiana na kila neno na moyo wa sheria kuu ya nchi,yaani katiba. 

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Abdul-Rahman