Wahariri wa magezeti juu ya kuisaidia Ugiriki | Magazetini | DW | 28.02.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Wahariri wa magezeti juu ya kuisaidia Ugiriki

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia uamuzi uliopitishwa na Bunge la Ujerumani wa kuupitisha mpango wa pili wa kuisaidia Ugiriki.Lakini wana mashaka kwa sababu bado pana upinzani.

Wabunge wa Ujerumani wakiupitisha mpango wa kuiokoa Ugiriki.

Wabunge wa Ujerumani wakiupitisha mpango wa kuiokoa Ugiriki.

Wabunge 496 waliupitisha na wengine 90 walipinga. Licha ya idadi hiyo kubwa ya wabunge kuukabali mpango huo ,wahariri wa magazeti katika maoni yao wanasema bado pana wasi wasi mkubwa. Gazetila "Markische Allgemeine" linatilia maanani kwamba wabunge wa vyama vilivyounda serikali ya mseto hawakuonyesha mshikamano thabiti na Mwenyekiti wao Kansela Markel.

Gazeti la "Die Welt" pia halina imani kubwa juu ya mpango huo wa pili wa kuiokoa Ugiriki na linasema katika maoni yake kwamba Wabunge wa Ujerumani wameupitisha mpango wa kuidhamini Ugiriki wenye uzito wa Euro Bilioni 130 huku nyuso zao zikikunjamana.Sababu ni kwamba mpango huo utamlemea mlipa kodi na hivyo panatakiwa uwazi na ukweli juu yake.

Mahariri wa gazeti la "Handelsblatt"pia anatilia maanani umuhimu wa kuwepo uwazi juu ya mpango wa kuisaidia Ugiriki Mhariri huyo anasema Kansela Merkel anajibu swali juu ya sababu ya kuisaidia Ugiriki katika msingi wa hisia. Lakini ,kwa manufaa ya kujenga imani, ingekuwa bora iwapo Kansela Merkel angeliwaambia wananchi wake ukweli.

Gazeti la "Hessiche/Niedersächsische" linasema wazi katika maoni yake kwamba, kwa mara nyingine Ujerumani inayatosa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Umoja usiokuwa na ufanisi. Mhariri wa gazeti hilo anasema Ujerumani inamwaga fedha kwa ajili ya kuuokoa Umoja wa Ulaya usiofanya kazi. Gharama za kuubeba Umoja huo ni kubwa sana.

Mhariri wa "Nordwest Zeitung" anakumbusha kwamba uchumi wa Ugiriki una ukubwa sawa na ule wa jimbo la Hesse la nchini Ujerumani. Sasa inakuaje kufilisika kwa jimbo hilo kusababishe uchumi wa dunia uanguke?

Wahariri wa magezeti ya hapa nchini leo pia wanazungumzia juu ya kinachotuhumiwa kuwa jaribio la kumuua mgombea urais nchini Urusi, Vladimir Putin.Gazeti la "Neue Presse" linasema katika vyombo vya habari vya Urusi mtu anasoma takriban taarifa juu ya Bwana Putin tu. Gazeti linaeleza kuwa wagombea wa vyama vya upinzani hawapewi fursa. Lakini nguvu za kisiasa za Putin zinatetereka ,sambamba na umaarufu wake. Kama siyo hivyo, basi ni vigumu kuelewa kwa nini, kabla ya uchaguzi jumapili ijayo,idara za usalama zimeshatoa taarifa juu ya watuhumiwa wa jaribio la kumuua Bwana Putin.

Gazeti la "Neue Presse" linahoji kuwa hayo yanathibitisha tuhuma kwamba wananchi wanawekwa katika hali ya wasiwasi juu ya kutokea vurumai, ili kuweza kusema kwamba ni Putin tu anaeweza kuiepuesha hali hiyo.

Mwandishi:Mtullya Abdu: (Deutsche Zeitungen.)

Mhariri: Yusuf Saumu