Wahariri wa magazeti watoa maoni juu ya Ujerumani kuipa Israel nyambizi
5 Juni 2012Juu ya mgogoro wa madeni gazeti la "Neue Presse" linasema kwamba sasa linahitajika suluhisho la Ulaya, yaani sera ya kiuchumi ya pamoja na hatimaye umoja wa kisiasa. Na hatua ya pili ni kwa nchi zote za Umoja wa sarafu ya Euro kushikamana ili kuyakabili madeni.
Gazeti la "Wiesbadener Kurier" linatilia maanani kwamba katika juhudi za kuukabili mgogoro wa madeni mabenki yamepunguza mikopo.Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba mabenki yamepunguza mikopo kwa kiwango kama kile, baada ya benki ya Lehman kusambaratika. Hiyo ni ishara ya mbiu ya mshikamano wa eneo la Umoja wa sarafu ya Euro. Nchini Ujerumani dalili za mabenki kuipunguza mikopo bado hazijaonekana. Hatahivyo uchumi wa Ujerumani umezingwa zingwa katika uekezaji vitega uchumi. Kinachopasa kufanya sasa ni kusubiri ishara thabiti kutoka Marekani na China. Pia inapasa kusubiri kuona jinsi wagiriki watakavyopiga kura. Lakini haidhuru matokeo hayo yatakuwaje, mustakabal wa sarafu ya Euro unahitaji msingi imara wa umoja wa kisiasa barani Ulaya.
Gazeti la "Mitteldeutsche Zeitung" linazungumzia juu ya uamuzi wa Ujerumani wa kuipa Israel nyambizi inayoweza kutumia silaha za nuklia. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza sababu ya Ujerumani kuupitisha uamuzi huo. Israel ni nchi yenye eneo dogo sana. Ndiyo kusema inaweza kuteketezwa kwa mabomu machache tu ya nyuklia. Na kwa hivyo ili kujihami inahitaji kuwa na nyambizi ya nyukulia ili kuwafanya maadui zake asilani wasithubutu kuishambulia. Huo ndio utakuwa usalama wa uhakika kwa Israel, endapo nchi ya kiadui kama Iran siku moja itamiliki bomu la nyuklia.Kwa hiyo hatua ya Ujerumani ya kuipa Israel nyambizi, siyo uamuzi wa kuipa nchi hiyo silaha ya kivamizi.
Malkia Elizabeth wa 2 ameadhimisha miaka 60 ya utawala wake nchini Uingereza.Katika muda huo wote Malkia huyo ameonyesha nidhamu ya hali ya juu. Lakini gazeti la "Badische Neueste Nachrichten" linauliza jee ni mpaka lini, na linasema kuwa Malkia Elizabeth ameonyesha nidhamu thabiti.Wakati wote amejihesabu kuwa ni mtumishi wa nchi.Katika nyakati za migogoro kama sasa ni jambo la kutia moyo kuona msimamo kama huo.Lakini sasa limebakia swali,jee ni mpaka lini. Uingereza pia haipo nje ya nyakati. za dunia
Mwandishi:Mtullya Abdu/
Duetsche Zeitungen/
Mhariri: Othman,Miraji