1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 80 wameokolewa, wawili wafa pwani ya Libya

Sudi Mnette
18 Februari 2024

Zaidi ya wahamiaji 80 wameokolewa, na wawili wamefariki dunia huku watatu wakiwa hawajulikani walipo katika zoezi la uokoaji lililofanywa kwenye bahari ya Mediterania karibu na pwani ya Libya.

https://p.dw.com/p/4cYE3
Marekebisho  ya  sewra ya uhifadhi katika Umoja wa Ulaya
Wahamiaji wanaokolewa na boti ya timu ya uokoaji ya MSF, baada ya kuondoka Libya wakijaribu kufikia ardhi ya Ulaya, katika Bahari ya Mediterania, Ijumaa, Oct. 6, 2023.Picha: Paolo Santalucia/picture alliance/AP

Shirika la misaada la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), limesema wahamiaji hao waliawaambia waokoaji kuwa wamelazimika kuogelea baada ya boti waliyokuwamo kuingia maji, ambapo wameongeza kuwa katika tukio hilo wenzao watatu walisalia katika boti hiyo na haijulikani walipo.Wahamiaji wamekua wakitumia miongoni mwa inayoelezwa kuwa ni njia hatari zaidi ulimwenguni ya uhamiaji, ya kuvuka bahari ya Mediterania wakitokea Afrika Kaskazini na kuingia Italia au Malta kwa kutumia vyombo vya usafiri visivyo salama. Ripoti iliyotolewa na Shirika la Uhamiaji, mwaka jana pekee takribani wahamiaji 2,500 waliotumia njia hiyo ya bahari walikufa au kutojulikana walipo.