1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa wa Kipalestina waachwa huru.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWJZ

Jerusalem. Israel imewaacha huru wafungwa 429 wa Kipalestina katika kuimarisha utawala wa rais Mahmoud Abbas kufuatia juhudi za amani zilizozinduliwa katika mkutano kuhusu amani ya mashariki ya kati mjini Annapolis. Wafungwa walichukuliwa hadi katika kituo cha upekuzi nje ya mji wa ramallah katika eneo la ukingo wa magharibi, ambapo baadaye waliingia katika maeneo ya Palestina. Wafungwa wote ni wanachama wa chama cha Fatah.