Wafuasi wa ″Uamsho″ wafikishwa mahakamani Zanzibar | Matukio ya Afrika | DW | 23.07.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Wafuasi wa "Uamsho" wafikishwa mahakamani Zanzibar

Kufuatia vurugu zilizotokea siku ya Ijumaa (20 Julai 2012) mjini Zanzibar kati ya jeshi la polisi na wafuasi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho, polisi imewakamata watu 43 na leo wanawafikisha mahakamani.

Jeshi la polisi ikiwatawanya watu wanaofanya vurugu.

Jeshi la polisi ikiwatawanya watu wanaofanya vurugu.

Waumini wa Kiislamu mjini Zanzibar walikuwa wanaendesha dua ya kuwaombea waliopoteza maisha katika ajali ya meli ya MV. Skagit iliyotokea wiki iliyopita, lakini polisi inasema walikuwa waumini hao walikusanyika kinyume na sheria na hivyo kusababisha vurugu katika mitaa ya Unguja mjini.

Amina Abubakar amezungumza na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed. Kusikiliza mazungumzo hayo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada