1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

wafuasi wa Laurent Nkunda waendelea kuzusha hofu Kongo

30 Agosti 2007

Wanajeshi tisa wa serikali ya Kongo wameuwawa baada ya kuvamiwa na kundi kubwa la waasi wa Nkunda

https://p.dw.com/p/CB1d
Picha: AP

Wanamgambo hao wanaomuunga mkono Kiongozi wa waasi Laurent Nkunda waliwavamia na kuwashambulia wanajeshi hao huko mashariki mwa jimbo la Kivu kaskazini.

Takriban wanamgambo 900 waliwavamia wanajeshi wa serikali katika eneo la Rubaya kiasi kilomita 60 kutoka mji wa Goma.