Wafaransa wafungwa jela kwa kujaribu kuiba watoto.
27 Desemba 2007Matangazo
Ndjamena.
Mahakama nchini Chad imewahukumu Wafaransa sita wafanyakazi wa shirika la kutoa msaada kwenda jela miaka minane na kazi ngumu, baada ya kuwapata na hatia ya kujaribu kuwateka nyara watoto 103 kutoka nchi hiyo ya Afrika. Watu hao sita raia wa Ufaransa kutoka katika shirika la kutoa huduma za kiutu la Zoe’s Ark walikamatwa Oktoba mwaka huu kwa kujaribu kuwachukua watoto kwenda nao Ufaransa, wote wakiwa chini ya umri wa miaka 10.