1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafadhili watakiwa waheshimu ahadi zao kwa Wapalestina

22 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cf5b

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limewatolea mwito wafadhili walioahidi kutoa zaidi ya dola bilioni saba kuwasaidia Wapalestina kwenye mkutano uliofanyika wiki hii mjini Paris Ufaransa, watimize ahadi zao haraka iwezekanavyo.

Naibu katibu mkuu anayehusika na maswala ya siasa, B Lynn Pascoe, amesema miezi michache ijayo ni muhimu katika juhudi za kuyafufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Wapaleswtina.

Fedha hizo zinanuiwa kuufua uchumi wa Palestina na kuiimarisha serikali ya rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas, inaoungwa mkono na nchi za magharibi.

Chama cha Fatah cha rais Abbas ambacho kinatawala eneo la ukingo wa magharibi wa mto Jordan, bado kinapingana na chama cha Hamas kinacholitawala eneo la Ukanda wa Gaza.