Wademokrats wanapinga kutumwa wanajeshi zaidi wa Marekani nchi i Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wademokrats wanapinga kutumwa wanajeshi zaidi wa Marekani nchi i Irak

Washington:

Wademokrats wanaodhibiti wingi wa viti katika baraza la Congress la Marekani wanapinga mpango wa rais George W. Bush wa kuzidisha idadi ya wanajeshi wao nchini Marekani.Uamuzi wa kutumwa wanajeshi zaidi utahatarisha maisha zaidi ya wamarekani-wamesema Herry Reid ambae ni mkuu wa kundi la wademokracts katika baraza la Senet na spika wa baraza la wawakilishi bibi Nancy Pelosi katika risala yao kwa rais George W. Bush.Wademokrats wanahoji pia wanajeshi zaidi watapindukia uwezo wa kijeshi nchini Irak.Jukumu kuu la wanajeshi wa Marekani litakua kuwapatia mafunzo wanajeshi wa Irak na sio kusaidia katika nyanja za mapigano.Wademokrats wameeleza kinaga ubaga pia rais George W. Bush hana tena haki ya kupitisha maamuzi bila ya idhini ya baraza la Congress.Kwa mujibu wa gazeti la New-York Times,rais George W. Bush anafikiria kutuma wanajeshi kati ya 17 elfu na 20 elfu wa ziada nchini Irak.Duru za kuaminika za serikali zinasema rais Bush atatangaza mkakati mpya wa serikali yake kuelekea Irak jumanne ijayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com