1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wademokrat wadhibiti tena baraza la wawakilishi Marekani

7 Novemba 2018

Wademokrat wamerejesha udhibiti wa baraza la wawakilishi kutoka kwa chama cha Rais Donald Trump kwenye uchaguzi wa katikati ya muhula, hatua inayoashiria kwamba itatatiza sera za Trump.

https://p.dw.com/p/37o3Q
Donald Trump
Picha: picture-alliance/dpa/AP/E. Vucci

Hatua ya WaDemrokrat kulidhibiti Baraza la Wawakilishi inafikisha kikomo cha udhibiti wa chama cha Republicana katika zaidi ya dazeni mbili za majimbo nchini Marekani. Hata hivyo bado matokeo ya viti kadhaa hayajatolewa, jambo ambalo huenda likasababisha wingi wa viti vya WaDemokrat kuongezeka hata zaidi. Mpaka sasa Wademcrat walikuwa wameshinda viti 221 dhidi ya 193 vya Republican.

Kwa kuwa na wingi wa viti, WaDemokrat watasimamia kamati kuu mbalimbali na kuwa na nguvu ya kutaka kupewa maelezo ya ulipaji kodi ya Rais Trump pamoja na kuchunguza uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2016, vile vile kumsaidia Trump katika kampeni zake.

Nancy Pelosi
Kiongozi wa Demokrat Nancy Pelosi akifurahia matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhulaPicha: Reuters/A. Drago

Kiongozi wa chama cha Democrat Nancy Pelosi ameutaja ushindi huo kuwa mwamko mpya wa Marekani. Nancy amesema,´´Bunge la Demokrat litatafuta suluhu ambalo litatuleta pamoja kwa sababu sote tumeshuhudia mgawanyiko nchini Marekani. Wamarekani wanataka amani. Wanataka matokeo. Wanataka sisi kufanya kazi ili kupata matokeo mazuri yatakayobadilisha maisha yao.´´

Kulingana na utafiti uliofanywa na Shirika la Habari la Associated Press, asilimia ishirini na tano ya wapiga kura walitaja masuala ya afya na uhamiaji kuwa muhimu katika uchaguzi huo. Kadhalika umeonyesha kuwa wapiga kura walimchukulia Trump kuwa sababu ya wao kupiga kura.

USA Trump Yellowstone International Airport
Picha: Reuters/C. Barria

Wakati huo huo Rais Donald Trump ameonekana kujigamba baada ya chama chake cha Republican  kusalia na viti vingi katika Baraza la Senate, licha ya udhibiti wake katika Bunge hilo kuonekana kuyumba. Warepulican walikuwa na viti 51 katika baraza hilo dhidi ya 45 vya Wademocrat, huku vikisalia viti vinne.

Kwa ujumla kulingana na utafiti wa uchaguzi  huo,  wapiga kura sita miongoni mwa kumi walisema kwamba Marekani inaelekea pabaya, lakini wengine wakautaja uchumi wa nchi hiyo kuwa bora au mzuri. Uchaguzi huu wa katikati ya muhula limeweka wazi usahihi wa wapiga kura katika masuala ya kabila, jinsia na elimu , na huenda ikarekebisha sura ya siasa za Marekani katika miaka ijayo.

Mwandishi: Sophia Chinyezi/APE

Mhariri: Iddi Sessanga