1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waaustralia wapiga kura leo

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSgS

Raia wa Australia wanapiga kura leo kulichagua bunge jipya. Kura ya maoni ya hivi karibuni inaonyesha kuwa chama cha Labour kinachoongozwa na Kevin Rudd huenda kikamshinda waziri mkuu, John Howard, na muungano wake wa kihafidhina wa Liberal National Coalition.

Kevin Ruud ameahidi kusaini mkataba wa Kyoto kuhusu ongezeko la joto duniani na kuwaondoa wanajeshi wa Australia walio nchini Irak.

Waziri mkuu John Howard amekuwa madarakani kwa miaka 11 na ana matumaini ya kushinda awamu nyengine ya tano. Amesema iwapo atashinda, atajiuzulu baada ya miaka miwili na akabidhi madaraka mwa waziri wa fedha, Peter Costello.