1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi walenga meli za Magharibi katika bahari ya Shamu

Amina Mjahid
7 Aprili 2024

Waasi wa Houthi wa Yemen wamesema wamerusha makombora na ndege za droni kwa meli za Uingereza, Marekani na Israel, hili likiwa ni shambulio la hivi karibuni kupinga vita vya Israel dhidi ya Hamas katika ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4eWAZ
Golf von Aden |
Meli iliyoshambuliwa katika Ghuba ya Aden Picha: Khaled Ziad/AFP/Getty Images

Kundi hilo linaloungwa mkono na Iran limesema limelenga meli za Uingereza na Marekani katika Bahari ya Shamu na  katika bahari ya kiarabu na Bahari Hindi walishambulia meli mbili za  Israeli zilizokuwa zinaenlekea katika bandari ya Israel. 

Msemaji wa waasi hao Yahya Saree alisema operesheni hiyo ilichukua saa 72 bila kutoa maelezo zaidi juu yake. 

Houthi imeongeza mashambulizi kwenye Bahari ya Shamu tangu kuanza kwa vita vya Israel na Hamas

Awali kampuni binafsi ya usalama ya Ambrey ya uingereza ilisema ilipata taarifa inayosema kwamba meli yake imeshambuliwa siku ya Jumalipi katika Ghiba ya Aden maili 102 kuelekea Kusini Magharibi mwaka eneo la Mukalla nchini Yemen.