Waandishi watishwa huko Gaza
31 Desemba 2007Matangazo
Waandishi kadhaa wa habari katika Ukanda wa Gaza wamepigiwa simu na watu wasiojulikana hii leo wakionywa wasiripoti juu ya mkutano wa hadhara wa chama cha Fatah unaotarajiwa kufanyika hapo kesho mjini Gaza.
Kitisho hicho kimesababisha hofu kwamba kundi la Hamas linalolidhibiti eneo la Ukanda wa Gaza linajaribu kuvikandamiza vyombo vya habari visiripoti kuhusu mkutano wa chama hasimu cha Fatah.
Kundi la Hamas limeupiga marufuku mkutano huo unaoelenga kuadhimisha miaka 43 tangu chama cha Fatah kilipoasisiwa.