Waandamanaji wameshambuliwa nchini Yemen
30 Mei 2011Matangazo
Vikosi vya usalama nchini Yemen viliwashambulia waandamanaji katika mji uliopo kusini,Taiz hapo jana na kuwaua watu 4 na kuwajeruhi wengine 90.
Maafisa katika hospitali wamesema vikosi hivyo vya usalama vinavyomuunga mkono rais Ali Abdullah Saleh, viliwashambulia kwa silaha waandamanaji.
Mapema hapo jana upinzani nchini humo na waziri wa zamani wa ulinzi aliyejiuzulu serikalini, jenerali Abdullah Ali Aleiwa, walimlaumu rais huyo kwa kuuruhusu mji uliopo kusini, Zinjibar, kuanguka mikononi mwa kundi la kigaidi la Al Qaeda, ili ayashawishi mataifa ya magharibi yamruhusu asalie madarakani.
Mwandishi:Maryam Abdalla/Afp/Rtre.