1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama ndugu vya kihafidhina vyashinda chaguzi za kijimbo

Tatu Karema
9 Oktoba 2023

Wapiga kura katika majimbo mawili nchini Ujerumani, Bavaria na Hesse, wamevipa ushindi vyama vya Christian Social Union CSU na Christian Democratic Union katika chaguzi za kijimbo zilizofanyika Jumapili (8.09.2023)

https://p.dw.com/p/4XH4f
Waziri Mkuu wa zamani wa Jimbo la Hessenn Volker Bouffier (kushoto) wa chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union (CDU) wakifuatilia matokeo ya kura  na wanachama wa CDU katika Bunge la Jimbo la Hessen huko Wiesbaden, Magharibi mwa Ujerumani
Waziri mkuu wa zamani wa Jimbo la Hessenn Volker Bouffier (kushoto) wa chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union (CDU) pamoja na wanachama wenzakePicha: KIRILL KUDRYAVTSEV/AFP

Chama cha mrengo mkali wa kulia cha Alternative for Germany, AfD pia kilizidi kujiimarisha, hii ikiwa ni kwa mujibu wa matokeo ya awali. Vyama vyote vitatu vinavyounda serikali ya muungano inayoongozwa na Kansela Olaf Scholz, yaani SPD, chama cha Kijani na FDP kinachowakilisha maslahi ya wafanyabiashara, vimefanya vibaya.

AFD yapinga vikali wahamiaji

Waziri kiongozi wa jimbo la Bavaria Markus Soeder kutoka chama cha CDU, amesema matokeo ya uchaguzi wa majimbo hayo mawili ni ishara kwamba raia wa Ujerumani wanataka sera mpya na imara zaidi kuhusu wahamiaji. Chama cha AfD kilichoshika nafasi ya pili baada ya wahafidhina katika chaguzi hizi, kinapinga vikali wahamiaji.