Viumbe wa porini wanakabiliwa na kitisho
Wakati baadhi ya viumbe wakikabiliwa na kitisho cha kutoweka kwa sababu ya ujangili, aina nyingine wameokolewa kutokana na jitihada za wataalamu wa wanyamapori . Mkutano wa wanyamapori utaamua hatma ya baadhi ya viumbe.
Njia ya kuelekea kutoweka
Mahitaji ya pembe za Faru hususani barani Asia umepelekea mnyama huyu kuelekea kutoweka. Licha ya biashara ya pembe za Faru kupigwa marufuku chini ya CITES tangu 1977, karibu faru 25,600 pekee kutoka aina zote tano za faru wamesalia . Katika hoja yenye utata, mfalme wa Swaziland anapendekeza kuhalalishwa kwa biashara ya kimataifa ya pembe za faru.
Janga la pembe za ndovu
Licha ya idadi ya tembo wa Afrika kupatwa na janga kwa kupungua kwa karibu theluthi moja kutoka 2007 hadi 2015 kwasababu ya biashara ya pembe za ndovu, Zimbabwe na Namibia zinapendekeza kuhalalishwa kwa biashara hiyo, katika jitihada za kupunguza mahitaji. Karibu tembo 27,000 wanakadiriwa kuuawa na majangili kila mwaka.
Ishara ya porini
Simba wa Afrika bado hachukuliwi kama aina ya mnyama aliye katika kitisho chini ya CITES, hata hivyo baadhi ya makundi kama Humane Society International yamependekeza mnyama huyo kuongezewa ulinzi kwa kuwa simba wa porini wamesalia kwa idadi ndogo karibu 20,000 barani Afrika.Pendekezo hilo hivi sasa linapingwa na nchi nyingi ikiwemo Umoja wa Ulaya. .
Nafasi ya juu kwenye orodha
Kakakuona ni mnyama mwenye hadithi ya kusikitisha kwa kuwa ni mnyama wa porini anayeongoza kwa kusafirishwa. Magamba yake yanatumiwa katika tiba za asili hasa nchini China na ni hazina kwa majangili. Wakati aina zote nane za Kakakuona zipo katika kitisho cha kutoweka, baadhi ya washiriki wa mkutano wa CITES CoP17 wanaunga mkono pendekezo la kudhibiti biashara ya mnyama huyo.
Chaza mzuri
Ingawa Chaza mwenye rangi huvutia na kuleta hali ya bahari nyumbani kwako lakini kitendo hiki kinachangia kutoweka kwa aina hii ya mnyama asiye wa kawaida wa baharini. Wanyama hawa wa pekee wa baharini pia wana sehemu yao, ni miongoni mwa mapendekezo 62 katika mkutano wa CITES CoP17, wataalamu wanataka ulinzi zaidi wa konokono wakubwa.
Faru anayeruka
Ndege huyu wa kushangaza ana muundo wa kofia kichwani mwake unaokadiriwa kuchukua asilimia 11 ya uzito wake kilo 3. Wakati mnyama huyu anatumia mdomo wake katika mapambano ya kichwa kwa kichwa na wanaume, binadamu anaitumia kama nyenzo ya kuchongea. Idadi kubwa ya ndege hawa barani Asia imewekwa katika kiambatanisho I lakini Indonesia inaomba ulinzi zaidi wa kiumbe hiki.
Wanyamapori pia ni kijani
Mimea imekuwa haipewi kipaumbele katika mijadala ya biashara ya wanyamapori. Hata hivyo CoP17 inashughulikia pia matatizo yanayoendana na biashara halali na haramu ya magogo kote duniani ambayo inatishia aina mbalimbali ya miti. Kwa mfano mahitaji ya kibiashara katika bara la Asia ya mbao zenye thamani za Rosewood, kumechochea mtandao mkubwa wa uhalifu.