Vitu 5 vinavyoweza kutunga muziki
Wanamuziki wanajua: Sauti inaweza kupatikana karibu kwa kila kitu. Ala za muziki hutengenezwa kutokana na vitu chungu nzima kama vile barafu au aisikirimu
Ala kutokana na barafu au aiskrimu
Sauti kutokana na barafu ni maalum na ina mahadhi tele. Wengi huirejelea sauti hiyo kuwa ya kipee. Kila mwaka katika tamasha, maelfu ya wageni hufurahia sauti ya barafu kwenye muziki. Wasanii hutumia zaidi ya masaa 12 kutengeneza ala kutokana na barafu. Lakini swali la ikiwa ala hizo hudumu hadi tamasha linapokamilika ni suala la bahati.
Tungo kutokana na vifaa vya kawaida
Midundo yake ni ya kukatika: James Provan ni msanii wa video anayejiita katika YouTube kama "Gir2007". Kutokana na ala zake zisizo za kawaida, vidio zake zimetazamwa mara zaidi ya milioni 17. Kwa mfano kwenye vidio yake itwayo "House Beat", ameigeuza nyumba nzima ya wazazi wake kuwa ala ya muziki.
Nyimbo kutokana na disketi ya kompyuta
Pawel Zadrozniak ambaye ni raia wa Poland anatumia sauti kutokana na sehemu za kompyuta kama vile 'hard drive, sehemu za kuingiza disketi na mitambo ya scanner kutunga muziki. Anapanga na kuzichanganya sauti hizo pamoja na midundo yao ili kupata mdundo anaotaka. Anaiita ala yake "Floppotron". Inaweza kutumika vyema katika wimbo wa Nirvana "Smells Like Nerd Spirit"
Ala za marumaru
Muimbaji Martin Molin kutoka Sweden alitengeneza ala yake ya muziki kutokana na marumaru kwa kipindi cha miaka 2. Ala hiyo ya mbao imejumuisha gololi 2,000 za chuma na husonga kwa mfumo maalum unaounda ala itoayo sauti. Ala hiyo ilisambaa kwa kasi katika mitandao na zaidi ya watu milioni 40 wameitizama.
Sauti kutokana na mboga
Je karoti itakuwaje filimbi? Kwa kutumia kisu na kifaa cha kutobolea! Bendi ya Vienna hugeuza boga kuwa ngoma, figili kuwa gitaa na pilipili kuwa pembe. Ili kuweza kutunga muziki lazima mboga ziwe mbichi. Bendi hiyo imekuwa ikiwatumbuiza watu ulimwenguni tangu 1998. Baada ya kila burudani, mboga hizo hupikiwa wageni