1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

211210 Visa Missbrauch Warndatei

Sekione Kitojo21 Desemba 2010

Balozi kadha za Ujerumani zimekuwa zikitoa visa kinyume na sheria tangu mwaka 2007. Balozi zinazolengwa zaidi katika kadhia hii ni ubalozi ulioko mjini Cairo.

https://p.dw.com/p/zo4t
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle.Picha: AP

Katika  balozi  kadha   za  Ujerumani  kuanzia  mwaka  2007 kumekuwa  kukitolewa    visa  za  kusafiria  kinyume  na  sheria. Taarifa   hizo  zimetolewa  kwanza  mwishoni  mwa  juma  na kuthibitishwa    siku  ya  Jumatatu  tarehe  20.12.  Ubalozi unaozungumziwa  sana  katika  taarifa  hii  ni  wa  Misr. Hali  hiyo inakumbusha  tukio  ambapo  serikali  ya  wakati  huo  ya  chana cha  SPD  na  Kijani  viliunda  tume  ya  bunge  kuchunguza  suala hilo.

Msemaji  wa  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani  Guido Westerwelle  hakuweza  kutambua  matamshi  yake   kuwa hayakubaliani. Kuna   baadhi  ya  matukio  yanapita  bila   kuonekana , anaeleza  Andreas  Paeschke, kwamba   katika  utaratibu   mkali wa  udhibiti  katika   wizara  ya   mambo  ya  kigeni  kuna tokea  hali kama  hiyo. Lakini   kutokana  na  kuwapo  karibu  maombi  milioni mbili   ya  visa   kila  mwaka    ni  wazi  kwamba  matatizo  kama haya  yanaweza  kutokea ,amesema  Paeschke.

Polisi  na  mwanasheria  mkuu  wa  serikali  ya  Ujerumani  kwa pamoja  katika  maelezo  yao   tangu  mwaka  2007  wamesema kuna  kazi  kubwa  ya  kufanywa, hususan  katika  kile kinachoshukiwa  kuwa  ni  utaratibu  kinyume  na  sheria  wa  utoaji wa  visa  katika  ubalozi  wa  Ujerumani   mjini  Cairo, lakini  pia katika  balozi  nyingine  za  kigeni.

Ni  suala  linalohusu  baadhi  ya  maombi  yanayofikia  100  ya  visa, ambayo  yako  katika  misingi  isiyoeleweka.  Katika  matukio mengine  ni  maombi  mawili, au  matatu.  Ni  matukio  yaliyotokea katika  bara  la  Afrika  ama  balozi  ndogo  katika   mashariki  ya kati, ni  katika  tukio  moja  tu  ambapo  nchi  ya  Ulaya  magharibi inahusika  katika  eneo  la  Balkan  na  jingine  limetokea  katika Asia  ya  kati. Katika  ripoti  za  vyombo  vya  habari  kuna  nchi  pia kama  za  Amerika  ya  kusini, lakini  hii  si kweli.

Wengi  wa  wafanyakazi  wanaofanyakazi  katika  balozi  hizo waliachiliwa  huru  baada  ya  kuhojiwa, anaeleza  msemaji  huyo  wa wizara  ya  mambo  ya  kigeni.

Wafanyakazi   wa  balozi, ambao  hutoa  huduma  za  kutoa  visa , hubadilishwa  mara  kwa  mara  katika  idara  ya  visa. Maombi  ya visa  hutawanywa  katika  idara  mbali  mbali  bila kuwapo  utaratibu maalum. Iwapo  kuna  shutuma  katika  mojawapo  ya  maeneo , mara  moja  hushughulikiwa  suala  hilo  kwa  pamoja   na  polisi  na mwendesha  mashtaka. Na  kama  ni  lazima  huchukuliwa  hatua mara  moja.

Matukio  ya  hivi  sasa  ya  utoaji  wa  visa  kinyume  na  sheria yanakumbusha  matukio  kama  hayo  yaliyotukia  mwaka  2004 katika  ubalozi  wa  Ujerumani   mjini  Kiev. Wakati  huo  kulikuwa  na maelfu  ya  wasafiri  ambao  walitiliwa  shaka  waliopewa  visa, ambapo  ilikuja  kugundulika  kuwa  ulikuwa  mtandao  wa  watu wanaosafirisha  watu  uliofaidika  na  kadhia  hiyo, ambapo  kulikuwa na  wafanyakazi  wa biashara  ya  ngono  ambao  ni  wa kulazimishwa  ambao  walisafirishwa  kuja  nchini  Ujerumani.

Mwandishi : Marcel Fürstenau / ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri : Abdul-Rahman

*