1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya wanakutana kujadili mizozo na usalama

Lilian Mtono
21 Machi 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels hii leo na kesho Ijumaa kwa ajili ya majadiliano juu ya vita vya nchini Ukraine na mzozo wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4dxpg
Brussels | Mpango wa Umoja wa Ulaya kuhusu Ukraine
Viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya walizindua mpango kuhusu Ukraine mapema wiki hii.Picha: Virginia Mayo/AP/dpa/picture alliance

Wakuu hao pia wataangazia mipango ya Halmashauri Kuu ya Ulaya ya kuiimarisha sekta yake ya ulinzi, pamoja na uwezekano wa baade wa kuupanua muungano huo wenye wanachama 27.

Marais pamoja na Mawaziri Wakuu aidha watatafakari juu ya mpango wa kununua silaha kwa ajili ya Ukraine kwa kutumia mapato ya mali zilizozuiwa za Urusi, kufuatia azimio lililoandaliwa na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atahutubia mkutano huo kwa njia ya video.

Kwenye mkutano huo aidha, viongozi hao kwa mara nyingine watatoa wito wa usitishwaji haraka wa mapigano katika Ukanda wa Gaza utakaowezesha makubaliano endelevu wa kusimamisha mapigano, hii ikiwa ni kulingana na rasimu ya taarifa iliyoonyeshwa shirika la habari la Ujerumani - DPA.