1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBosnia na Herzegovina

Ulaya kufanya mazungumzo na Bosnia juu ya kujiunga na EU

22 Machi 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubali kufanya mazungumzo na Bosnia kuhusu ombi la nchi hiyo kujiunga na Umoja huo.

https://p.dw.com/p/4e05N
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Bosnia na Herzegovina Borjana Krišto na Kamishna wa Umoja wa Ulaya Oliver Varhelji
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Bosnia na Herzegovina Borjana Krišto na Kamishna wa Umoja wa Ulaya Oliver VarheljiPicha: Council of Ministers of Bosnia and Herzegovina

Mazungumzo hayo yataanza mara baada ya nchi hiyo ya ukanda wa Balkan itakapopitisha mageuzi muhimu katika idara ya mahakama na mfumo wa uchaguzi.

Rais wa baraza la Ulaya Charles Michel ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa X, akiipongeza Bosnia na kueleleza kuwa nchi hiyo inakaribishwa kujiunga na familia ya Umoja wa Ulaya.

Soma pia: Uholanzi yaiomba radhi Srebrenica kwa mauaji 

Bosnia imepewa hadhi ya kuwa mgombea wa nafasi ya uanachama wa Umoja wa Ulaya tangu mwaka 2022 japo ilihitajika kufanya msururu wa mageuzi kabla ya mchakato huo kupelekwa katika hatua nyengine.

Wiki iliyopita, Umoja wa Ulaya ilisema kuwa nchi hiyo imepiga hatua japo haijafanya mageuzi katika idara ya mahakama na mfumo wa uchaguzi.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeuchochea msukumo wa Umoja wa Ulaya kutanua kuelekea Ulaya Mashariki na Kati. Mnamo mwezi Disemba, nchi wanachama zikikubaliana kuanza mazungumzo ya Ukraine na Moldova kujiunga na Umoja huo.