1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa riadha wapigwa marufuku ya maisha

8 Januari 2016

Maafisa wa zamani wa riadha wa shirikisho la Riadha la Kimataifa – IAAF, wamepigwa marufuku ya maisha katika mchezo huo kuhusiana na mashtaka ya rushwa

https://p.dw.com/p/1HaNP
Leichathletikfunktionäre Balakhnichev und Diack
Picha: Getty Images/S. Forster

Aliyekuwa mkuu wa shirikisho la riadha la Urusi Valentin Balakhnichev, aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya riadha Aleksey Melnikov, na Papa Massata Diack, mwanawe Rais wa zamani wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa – IAAF Lamine Diack, wote wamepigwa marufuku ya maisha katka mchezo huo kuhusiana na mashtaka ya rushwa.

Tume ya maadili ya IAAF pia imempiga aliyekuwa mkuu wa shirika hilo wa kupambana na dawa za kuongeza nguvu mwilini Gabrielle Dolle kwa miaka mitano, baada ya watu hao wote wanne kupatikana kukiuka sheria kadhaa za kupambana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuhusika na matukio ya kuficha matokeo ya vipimo vilivyoonyesha matumizi ya dawa hizo miongoni mwa wanariadha. Balakhnichev na Diack pia wamepigwa faini ya dola 25,000 na Melnikov 15,000.

Mwisho wa michezo kwa sasa, shukrani kwa kujiunga nami, kwa mengi zaidi basi tembelea dw.com/Kiswahili, na pia tuwasiliane kwenye facebook, na twitter. Kwaheri

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Sessanga