1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Afrika waomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II

Saleh Mwanamilongo
9 Septemba 2022

Viongozi barani Afrika leo wamejiunga na wenzao duniani kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza, wengi wakimtaja kuwa kiongozi wa mfano.

https://p.dw.com/p/4GcfV
UK Queen Elizabeth II gestorben
Picha: Markus Schreiber/AP/dpa/picture alliance

Viongozi barani Afrika leo wamejiunga na wenzao duniani kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza, wengi wakimtaja kuwa kiongozi wa mfano na anayeacha urathi utakaokumbukwa daima.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Senegal Macky Sall amesema amehuzunishwa na kifo cha Malkia Elizabeth na kuusifu utawala wake wa kipekee wa miaka sabini.

Nchini Malawi rais  Lazarus Chakwera amemwelezea Malkia Elizabeth kuwa rafiki wa nchi hiyo ujumbe uliotolewa pia na rais Gabon Ali Bongo.

Salamu nyingine za rambirambi zimetolewa na rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini.

Hata hivyo mwanasiasa kijana wa Afrika Kusini Julius Malema, amesema chama chake cha EFF hakiombolezi kifo cha Malkia Elizabeth, kwa sababu msiba huo ni kumbukumbu ya madhila ambayo Afrika imepitia katika historia yake.