1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi liachie madaraka ya Mali ndani ya mwaka mmoja

Sudi Mnette
29 Agosti 2020

Viongozi wa eneo la Afrika Magharibi wameutaka uongozi wa kijeshi wa Mali kutochukua zaidi ya mwaka mmoja kukabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia.

https://p.dw.com/p/3hiop
Mali Bamako Verhandlungen zwischen ECOWAS und Militärführern | Goodluck Jonathan
Picha: Reuters/M. Kalapo

 

Kauli hiyo wameitoa baada ya kufanya mkutano kwa njia ya vidio baada ya mkutano mwingine kama huo na wanajeshi waliofanya mapinduzi kushindwa kuzaa matunda. Wanajeshi hao ambao wanajiita kamati ya kitaifa ya ukombozi wa watu iliweza kutekeleza moja tu, kati ya matakwa ya viongozi wa kanda hiyo baada ya Alhamisi kumwachia huru Rais wa Zamani, Ibrahim Boubacar Keita, ikiwa zaidi ya wiki moja kutangaza kujiuzulu kwake kulikofuatiwa na mapinduzi.

Msimamo mkali wa wanajeshi wanaoongoza Mali

Mali I  Demonstration gegen Regionalblock ECOWAS in Bamako
Wanajeshi wa mali katika doriaPicha: Reuters/M. Kalapo

Hata hivyo wanajeshi ambo wanashika atamu ya uongozi, wamependekeza uchaguzi mwingine ufanyike 2023, jambo ambalo limekataliwa vikali na matiafa 15 yalio katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS. Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amelitaka jeshi kutii wito wa ECOWAS.

kiongozi huyo alisema"Watu wa Mali na viongozi wa kijeshi wanapaswa kukubali hali tete ya taifa lao na kitisho kinachoweza kuwakabili wananchi wa Mali pamoja na eneo la ECOWAS." Alisema Buhari katika taarifa yake. Baada ya mapinduzi kama haya ya sasa ya Mali, uchaguzi uliweza kufanyika katika kipindi cha miezi 18.

Pendekezo la kuundwa jeshi la pamoja la kurejesha utulivu

Hata hivyo tayari ECOWAS imeusimamisha uanachama wa Mali katika umoja huo, na pia kusitisha shuguhuli zake za maingiliano ya kibiashara.Mataifa jirani yamefunga mipaka na kutishia vikwazo zaidi katika jitihada viongozi wa kijeshi kufuata katiba.

Soma zaidi:Wanajeshi walioasi Mali wamuachia huru Boubakar Keita

Kundi la matafa la ECOWAS limetoa pendekezo la kuundwa kwa jeshi la dharura, kwa lengo la kwenga kufanikisha utawala wa kiraia, wazo ambalo hata hivyo linaonekana kupewa kisogo kutokana na raia wa taifa hilo kufanya maandamano na kuunga mkono kuondolewa rais wao waliemchagua kidemokrasia. Hata hivyo Rais wa Nigeria ameutaka utawala wa kijeshi kuwaachia huru maafisa wote wa serikali ambao bado wapo kizuizini.

Chanzo:APE