1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikwazo zaidi dhidi ya Iran vyaafikiwa

16 Machi 2007

Dola kuu 5 zanachama wa kudumu wa Baraza la usalama la UM wameafikiana vikwazo zaidi dhidi ya Iran kwa kutoitikia kwake kusimamisha mradi wake wa kinuklia.Azimio litapigiwa kura wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/CHI2

Dola kuu 5 wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UM pamoja na Ujerumani baada ya mvutano wa wiki kadhaa zimeafikiana sasa vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran kwa ajili ya kukataa kuachana na mradi wake wa kinuklia.

Marekani,Russia,China,Uingereza na Ufaransa ziliifikisha jana nakala ya azimio lao mbele ya Baraza la Usalama la UM.Haitazamiwi lakini kulipigia kura kabla kati ya wiki ijayo.

Azimio jengine dhidi ya Iran katika UM sasa liko njiani kupitishwa.Baada ya China kuridhia vikwazo hivyo,dola 5 zenye kura ya turufu –veto-zilishauriana na Ujerumani na baadae zikaliweka azimio lao mbele ya wanachama wengine wa Baraza la Usalama.

Katika azimio hili jipya kuna majina 12 m apya na makampuni 10 mapya yanayotakiwa kufungiwa akiba zao za banki,marufuku kwa Iran kuuza silaha zake n’gambo pamoja na kutakiwa nchi zanachama wa UM kuchukua hadhari katika kuiuzia Iran silaha.

Isitoshe, Iran isipewe mikopo mipya au kuichukulia dhamana ya mikopo hiyo.

Balozi wa Marekani Alejandro Wolff amesema mapendekezo hayo yote ndio yalioafikiwa kwa jumla.Anasema:

“Haya ndio mambo yote ambayo yakipitishwa na Baraza la Usalama , kwa muujibu wa maoni ya kundi la dola 6, ni hatua barabara ya kuifanya serikali ya Iran kuupokea mkono inayonyoshewa isimamishe kurutubisha madini ya uranium na kurejea katika meza ya mazungumzo.”

Hadi dakika ya mwisho China ikisitasita kuungamkono vikwazo hivyo.Marufuku ya silaha isiokamili na kuizuwilia serikali ya Iran kupata dhamana ya kuweza kujipatia mikopo,hakujaipendeza Beijing.

Kwa sasa mikopo kutolewa kwa makampuni yasio ya serikali ya Iran si marufuku .Halkadhalika, miradi ya serikali na ya kiutu na ya maendleo haijaguswa na vikwzao hivyo vinavyopendekezwa.

Bila shaka azimio hilo dhidi ya Iran, halitaweza kupitishwa wiki hii kama ilivyopendelea marekani.Kwani mara hii Baraza la Usalama halitaki kutiwa shindo na dola kuu zenye kura za veto kama ilivyotokea katika mkesha wa x-masi mwaka jana.hii ni kwa muujibu asemavyo mwenyekiti wa Baraza hilo la Usalama Bw.Kumalo:

“Niaminini .Mara hii, hakuna kupitisha mambo moja kwa moja.Kwanza, tutaipeleka nakala ya azimio hilo katika miji mikuu yetu na tutachukua muda tunaohitaji kuizingatia nakala hiyo na baadae duru ya wanachama 15 itaamua iwapo tunahitaji mabingwa au la na mwishoe, ndipo tutaipima hali ilivyo.”

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Usalama la Um akaongeza:

“Kwamba dola kuu 5 na Ujerumani ndizo werevu na zenye hikma na tilobaki sote kazi yetu ni kuidhinisha waliopitisha tu,hakuna aliesema hivyo.”

Vipi Iran imeitikia maafikiano ya dola hizo 6 ya kuiwekea vikwazo ?

Iran haikustuka .Iran haina wasi wasi-alidai rais wake Mahmoud Ahmadinejad wakati wa tafrija moja iliofanyika nchini Iran.Alisema hata vikwazo vikali zaidi havitaizuwia Iran kuendelea na mradi wake wa kinuklia.

Licha ya vikwazo ilivyowekewa siku za nyuma, Iran iliweza kujipatia ufundi wa teknolojia ya kinuklia ambao kwa muujibu wa mkataba wa kutoeneza silaha za kinuklia,Iran ina haki ya kujipatia na kuutumia.

Rais Ahmadinejad wa Iran, angependa binafsi uso kwa uso tena kinaganaga kuliambia baraza la Usalama huko huko New York kwa muujibu wa mwenyekiti wa Baraza hilo Bw.Kumalo mara tu likipitishwa.