1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya wapinzani wa Ujerumani barani Ulaya

22 Mei 2014

Mahasimu wakubwa wa Ujerumani barani Ulaya wamevichagua vikosi vyao vya mwanzo kwa ajili ya Dimba la Kombe la Dunia la 2014 nchini Brazil. Ni majina yepi hayo yanayomuumiza kichwa kocha Joachim Löw?

https://p.dw.com/p/1C3b6
UEFA EURO 2012 Tschechien vs Portugal Sieg
Picha: picture-alliance/dpa

Uhispania: Mabingwa hao wa Ulaya na Ulimwengu, wanajigamba kwa vipawa chungu nzima katika kikosi chao cha mwanzo. Huku safu ya kiungo ikiwajumuisha wachezaji kama vile Javi Martinez wa Bayern, na washambuliaji kadhaa wenye thamani kubwa ulimwenguni, bila shaka kutakuweko na nyuso zitakazokasirika wakati kikosi hicho kitakapopunguzwa hadi idadi inayostahiki ya wachezaji 23.

Kikosi cha mwanzo cha Uhispania: Walinda lango:Iker Casillas (Real Madrid), Jose Reina (Napoli), Davidde Gea (Manchester United); Mabeki:Cesar Azpilicueta (Chelsea), Gerard Pique (Barcelona),Sergio Ramos Real Madrid), Jordi Alba (Barcelona), Alberto MorenoSevilla), Javi Martinez (Bayern Munich), Raul Albiol (Napoli), Juanfran (Atletico Madrid), Dani Carvajal (Real Madrid); Viungo:Sergio Busquets (Barcelona), Xabi Alonso (Real Madrid), Koke (Atletico Madrid), Ander Iturraspe (Athletic Bilbao), Xavi(Barcelona) Thiago (Bayern Munich), Pedro (Barcelona), Jesus Navas (Manchester City), Cesc Fabregas (Barcelona), Santi Cazorla(Arsenal), Andres Iniesta(Barcelona); Washambuliaji:Diego Costa (Atletico Madrid), David Villa (AtleticoMadrid), Fernando Torres (Chelsea), Alvaro Negredo (Manchester City), Fernando Llorente (Juventus), David Silva (Manchester City), Juan Mata (Manchester United)

Hasimu mkubwa sana kimataifa wa Ujerumani na mwenye usumbufu ni Italia. Kikosi chao kina nyuso maarufu kama vile Andrea Pirlo na Gianluigi Buffon wote wa Juventus, na mshambuliaji matata wa AC Milan Mario Balotelli. Mshambuliaji Ciro Immobile, mwenye umri wa miaka 24 anayeripotiwa kumezewa mate na Borussia Dortmund, ameitwa kikosini baada ya kuifungia FC Torino magoli 22 katika Serie A msimu huu.

Magoli mawili ya Mario Balotelli katika nusu fainali ya Kombe la EURO yalivunja mioyo ya Wajerumani
Magoli mawili ya Mario Balotelli katika nusu fainali ya Kombe la EURO yalivunja mioyo ya WajerumaniPicha: AP

Kikosi cha mwanzo cha Italia: Walinda lango: Gianluigi Buffon (Juventus), Mattia Perin (Genoa), Salvatore Sirigu (Paris Saint Germain), *Antonio Mirante (Parma); Mabeki: Ignazio Abate (Milan), Andrea Barzagli (Juventus), Leonardo Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Matteo Darmian (Torino), Mattia De Sciglio (Milan), Christian Maggio (Napoli), Gabriel Paletta (Parma), Manuel Pasqual (Fiorentina), Andrea Ranocchia (Inter); Viungo: Alberto Aquilani (Fiorentina), Antonio Candreva (Lazio), Daniele De Rossi (Roma), Claudio Marchisio (Juventus), Riccardo Montolivo (Milan), Thiago Motta (Paris Saint Germain), Marco Parolo (Parma), Andrea Pirlo (Juventus), Romulo (Verona), Marco Verratti (Paris Saint Germain); Washambualiaji: Mario Balotelli (Milan), Antonio Cassano (Parma), Alessio Cerci (Torino), Mattia Destro (Roma), Ciro Immobile (Torino), Lorenzo Insigne (Napoli), Giuseppe Rossi (Fiorentina)

Ubelgiji imekitangaza kikosi imara, kichanga na pia chenye nyuso zinazofahamika katika Bundesliga. Kipa wa Hoffenheim Koen Casteels yuko ndani, pamoja na beki wa Bayern Munichs Daniel van Buyten na mshambuliaji wa Wolfsburg Kevin de Bruyne. Wanajiunga na kikosi imara chini ya uongozi wa bingwa wa Premier Legaue ya England, Vincent Kompany.

Kikosi cha mwanzo cha Ubelgiji: Walinda lango: Thibaut Courtois (Atletico Madrid - on loan from Chelsea), Simon Mignolet (Liverpool), Koen Casteels (Hoffenheim), Silvio Proto (RSC Anderlecht); Mabeki: Toby Alderweireld (Atletico Madrid), Anthony Vanden Borre (RSC Anderlecht), Laurent Ciman (Standard Liege), Vincent Kompany (Manchester City), Daniel van Buyten (Bayern Munich), Thomas Vermaelen (Arsenal, Nicolas Lombaerts (Zenit St. Petersburg), Jan Vertonghen (Tottenham Hotspur); Viungo:Axel Witsel (Zenit St. Petersburg), Steven Defour (Porto), Marouane Fellaini (Manchester United), Moussa Dembélé (Tottenham Hotspur), Nacer Chadli (Tottenham Hotspur), Kevin De Bruyne (VfL Wolfsburg), Eden Hazard (Chelsea), Dries Mertens (Napoli), Kevin Mirallas (Everton), Adnan Januzaj (Manchester United); Washambulaiaji:Romelu Lukaku (Everton - on loan from Chelsea), Divock Origi (Lille OSC); Akiba: Radja Nainggolan (AS Roma), Sebastien Pocognoli (Hannover 96), Thorgan Hazard (Zulte Waregem - on loan from Chelsea), Guillaume Gillet (RSC Anderlecht), Michy Batshuayi (Standard Liege), Jelle van Damme (Standard Liege)

Uingereza, hasimu wa jadi wa Ujerumani, imeamua kukichagua kikosi chipukizi. Kufuatia mpango wa Ujerumani Kombe la Dunia katika mwaka wa 2006, kocha Roy Hodgson amemjumuisha beki wa Southampton mwenye umri wa miaka 18 Luke Shaw, pamoja na mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling (19) na chipukizi wa Everton Ross Barkley (20). Kigogo Ashley Cole amewachwa nje na hapo akaamua kustaafu kutoka soka ya kimataifa, baada ya kuichezea England mechi 107.

Roy Hodgson amesifiwa kwa kukichagua kikosi chipukizi
Roy Hodgson amesifiwa kwa kukichagua kikosi chipukiziPicha: picture alliance/Photoshot

Kikosi cha mwanzo cha England: Walinda lango: Fraser Forster (Celtic), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City); Mabeki: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Manchester United), Luke Shaw (Southampton), Chris Smalling (Manchester United); Viungo: Ross Barkley (Everton), Steven Gerrard (Liverpool), Jorden Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Southampton), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Jack Wilshere (Arsenal). Forwards: Rickie Lambert (Southampton), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United); Akiba: John Ruddy (Norwich City), Jon Flanagan (Liverpool), John Stones (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley (Manchester United), Andy Carroll (West Ham United), Jermain Defoe (Toronto FC).

Licha ya kufuzu kibahati katika dimba hilo kupitia mechi za mchujo, kikosi cha Ufaransa bado kinaashiria nguvu ya pamoja. Mchezaji wa Bayern Franck Ribery ni mmoja wa washambuliaji watano, huku kiungo wa Juventus Paul Pogba na Karim Benzema wa Real Madrid wakiwa katika hali nzuri kabla ya tamasha hilo. Kukosekana kwa majina ya Samir Nasri na Gael Clichy wa Manchester City kuliwashangaza wengi, pamoja na Yoann Gourcuff wa Olympique Lyon.

Kikosi cha mwanzo cha Ufaransa: Walinda lango: Mickael Landreau (Bastia), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille); Mabeki: Mathieu Debuchy (Newcastle), Lucas Digne (Paris St. Germain), Patrice Evra (Manchester United), Laurent Koscielny (Arsenal), Eliaquim Mangala (Porto), Bacary Sagna (Arsenal), Mamadou Sakho (Liverpool), Raphael Varane (Real Madrid); Midfielders: Yohan Cabaye (Paris St. Germain), Clement Grenier (Lyon), Blaise Matuidi (Paris St. Germain), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissokko (Newcastle), Mathieu Valbuena (Marseille); Washambuliaji: Karim Benzema (Real Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Real Sociedad), Loic Remy (Newcastle), Franck Ribery (Bayern Munich); Akiba: Remy Cabella (Montpellier), Maxime Gonalons (Lyon), Alexandre Lacazette (Lyon), Loic Perrin (Saint-Etienne), Stephane Ruffier (Saint-Etienne), Morgan Schneiderlin (Southampton), Benoit Tremoulinas (Saint-Etienne).

Uholanzi ambao walishindwa kaltika fainali ya mwaka wa 2010, wametuma ujumbe mkali katika kikosi kilichochaguliwa. Nahodha wa Ausgburg Paul Verhaegh ndilo jina linaloshangaza wengi. Majina makubwa ya Bundesliga Arjen Robben (Bayern Munich), Klaas-Jan Huntelaar (Schalke 04) na Rafael van der Vaart (HSV) bila shaka hayangekosekana.

Arjen Robben amewahi kucheza katika fainali ya Kombe la Dunia, lakini jee, anaweza kufika hapo tena?
Arjen Robben amewahi kucheza katika fainali ya Kombe la Dunia, lakini jee, anaweza kufika hapo tena?Picha: Reuters

Kikosi cha mwanzo cha Uholanzi: Walinda lango:Jasper Cillessen (Ajax), Tim Krul (Newcastle), Michel Vorm (Swansea), Jeroen Zoet (PSV Eindhoven); Mabeki:Daley Blind, Joel Veltman (both Ajax), Stefan de Vrij, Daryl Janmaat, Terence Kongolo, Bruno Martins Indi, Tonny Vilhena (all Feyenoord), Karim Rekik (PSV Eindhoven - on loan from Manchester City), Patrick van Aanholt (Vitesse Arnhem), Paul Verhaegh (FC Augsburg), Ron Vlaar (Aston Villa); Viungo:Jordy Clasie (Feyenoord), Jonathan de Guzman (Swansea), Nigel de Jong (AC Milan), Leroy Fer (Norwich), Arjen Robben (Bayern Munich), Wesley Sneijder (Galatasaray), Rafael van der Vaart (Hamburg), Georginio Wijnaldum (PSV Eindhoven); Washambuliaji:Jean-Paul Boetius (Feyenoord), Memphis Depay (PSV Eindhoven), Klaas-Jan Huntelaar (Schalke 04), Dirk Kuyt (Fenerbahce), Jeremain Lens (Dynamo Kiev), Quincy Promes (Twente), Robin van Persie (Manchester United).

Cristiano Ronaldo ndilo jina linaloongoza katika kikosi cha Ureno na linafuatwa na mwenzake katika Real Madrid, Fabio Coentrao, Joao Moutinho wa Monaco na chipukizi William Carvalho. Mshambuliaji wa Wolfsburg Vieirinha pia ametajwa huku Nani wa Manchester United labda akiwashangaza wengi kwa kujumuishwa.

Kikosi cha mwanzo cha Ureno: Walinda lango: Anthony Lopes (Lyon), Beto (Sevilla), Eduardo (Braga), Rui Patricio (Sporting); Mabeki: Andre Almeida (Benfica), Antunes (Malaga), Bruno Alves (Fenerbahce), Fabio Coentrao (Real Madrid), Joao Pereira (Valencia), Neto (Zenit), Pepe (Real Madrid), Ricardo Costa (Valencia), Rolando (Inter); Viungo: Andre Gomes (Benfica),Joao Mario (Vitoria), Joao Moutinho (Monaco), Miguel Veloso (Dinamo Kiev), Raul Meireles (Fenerbahce), Ruben Amorim (Benfica), William Carvalho (Sporting); Washambuliaji: Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Eder (SC Braga), Helder Postiga (Lazio), Hugo Almeida (Besiktas), Ivan Cavaleiro (Benfica), Nani (Manchester United), Rafa (Braga), Ricardo Quaresma (Porto), Varela (Porto), Vieirinha (Wolfsburg)

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Yusuf Saumu