Vikosi vya UN haviondoki!,asema Ban Ki Moon. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 19.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Vikosi vya UN haviondoki!,asema Ban Ki Moon.

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wataendelea kuyatimiza majukumu yao nchini Ivory Coast hata baada ya rais anayewania muhula mwengine Laurent Gbabgo kutoa wito wa kuwataka waondoke nchini humo.

default

Vikosi vya UN mjini Abidjan, Ivory Coast

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,ujumbe wa UNOCI ulioko nchini humo, utaendelea kutimiza wajibu wake nchini Cote d'Ivoire kwa minajili ya kuzuwia vitendo vyovyote vinavyochochea ghasia,chuki au mashambulio dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.Mapema hapo jana Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alimtolea wito Laurent Gbagbo kuachia ngazi na kumpa nafasi mpinzani wake mkuu.

NO-Flash Demonstrationen in Abidjan Elfenbeiküste

Wafuasi wa Alassane Ouattara:ghasia zimeigubika Ivory Coast kufuatia uchaguzi uliozua utata

Kauli hizo zimetolewa baada ya Laurent Gbagbo kuwataka wanajeshi hao kuondoka nchini humo kwa madai kwamba wanawaunga mkono waasi ambao ni wafuasi wa Alassane Ouatarra.Umoja wa Mataifa,Marekani,Umoja wa Ulaya pamoja na nchi jirani ya Ivory Coast wamemtolea wito Laurent Gbagbo kuachia madaraka kwa sababu anaendelea kunga'nga'nia ushindi kufuatia duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyozua utata.

DW inapendekeza

 • Tarehe 19.12.2010
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Qfkl
 • Tarehe 19.12.2010
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Qfkl

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com