Vikosi vya Rwanda vyaelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati
19 Januari 2014Matangazo
Jeshi hilo limeelekea Jamhuri ya Afrika ya kati likiwa na zana nzito nzito za kivita kama ishara ya kukabiliana na hali yoyote ya vita. Kikosi hicho kimesafiri kwa msaada wa helikopta ya kivita ya jeshi la Marekani.
Mwandishi wetu wa Kigali Sylvanus Karemera amefanya mahojiano na Msemaji wa jeshi la Rwanda Brigedia Jenerali Joseph Nzabamwita ambaye anaanza kwa kuthibitisha kuondoka kwa kikosi hicho na jukumu lake nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Sylvanus Karemera
Mhariri: Saumu Yusuf