Vikosi vimesababisha umwagaji damu mkubwa Yemen
19 Septemba 2011Matangazo
Watu walikusanyika kwa maelfu katika maandamano ya kumpinga rais wa muda mrefu, Ali Abdullah Saleh na serikali yake. Watu walioshuhudia mashambulio hayo wamesema, hadi watu 26 wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa. Waandamanaji walipojaribu kuelekea makao rasmi ya rais, vikosi vilifyatua risasi. Vile vile vilitumia maji na gesi ya kutoa machozi.
Licha ya kushinikizwa kuondoka madarakani, Rais Saleh anakataa kutia saini makubaliano ya kuwakabidhi wengine madaraka. Hivi sasa, kiongozi huyo yupo Saudi Arabia kwa ajili ya matibabu ya majeraha aliyopata katika mashambulio yaliyofanywa dhidi ya makao yake rasmi mjini Sanaa mnamo mwezi wa Juni.