Vigogo waondolewa katika hatua ya mtoano
2 Julai 2018Wenyeji Urusi walifanya kazi kweli kweli na kuwaondoa Uhispania kupitia mikwaju ya Penalti sawa na walivyofanya Croatia dhidi ya Denmark.
Mpaka sasa mechi mbili za robo fainali zimeshathibitishwa. Ijumaa tarehe 6 Uruguay watashuka dimbani dhidi ya Ufaransa, na kisha Jumamosi, tarehe 7, wenyeji Urusi watapambana na Croatia. Katika mechi nyingine mbili za robo fainali: Mshindi kati ya Brazil na Mexico atachuana na mshindi kati ya Ubelgiji na Japan. Kisha mshindi kati ya Sweden na Switzerland atamualika mshindi kati ya Colombia na England.
Baadaye leo usiku, Ubelgiji wataangushana na Japan ambayo ina ndoto ya kutinga robo fainali kwa mara yao ya kwanza kabisa. Narudi kwake Mtemi Ramadhan kupata tathmini yake, Mtemi, ni mechi ambayo ukiangalia kwenye karatasi, utajua tu ushindi ni wa Ubelgiji, lakini mechi za mwishoni mwa wiki, zimedhihirisha kuwa ukweli wa mambo unadhihirika uwanjani
Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Josephat Charo