1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIENNA:Watuhumiwa watatu waachiwa nchini Austria

Maafisa wa usalama nchini Austria wamewaachia watu watatu waliokamatwa kutokana na kutuhumiwa kutoa vitisho vya kuzishambulia Austria na Ujerumani.

Watu hao walituhumiwa kutoa vitisho hivyo katika ukanda wa video walioutangaza kwenye mtandao wa internet.

Msemaji wa mahakama nchini Austria ameeleza kuwa watu hao wameachiwa kwa sababu hapakuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha iwapo walitenda kosa lolote.Lakini watuhumiwa wengine wawili wataendelea kuwekwa mahabusu.

Watu hao walikamatwa baada ya idara za usalama nchini Ujerumani kuzuia mashambulio yaliyopangwa kufanywa na magaidi , kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani na kwenye uwanja wa ndege wa Frankfurt.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com