1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIENNA:Mazungumzo juu ya Kosovo

Viongozi wa Serbia na wajimbo la Kosovo watakutana leo hii mjini Vienna kwa ajili ya mazungumzo mapya juu ya hatma ya jimbo la Kosovo.

Hata hivyo inatabiriwa hakuna mwafaka utakaofikiwa kuhusu suala hilo.

Waziri mkuu wa Kosovo Agim Ceku akiwasili mjini Vienna Austria hapo jana alisema hakuna mengi ya kujadiliwa kwa sababu pendekezo lilitolewa na likaungwa mkono na wengi isipokuwa nchi mbili tu ambazo zinapinga uhuru wa jimbo hilo Urussi na Serbia kwa hivyo kwa upande wa Kosovo suala hilo limetatuliwa na hawatapoteza muda wa kujadili mambo ambayo hayatafikia mwafaka.

Walbania ambao ndio wakaazi wengi wa jimbo hilo la Kosovo wanadai uhuru wa jimbo lao baada ya kuwa chini ya sheria ya Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka minane lakini Serbia inasema kulipa uhuru jimbo hilo kutakuwa kukiuka sheria za kimataifa.Umoja wa mataifa umeweka muda wa mwisho wa hadi tarehe 10 Desemba kufikiwa mwafaka wa mazungumzo hayo muda ambao umepingwa na Urussi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com