1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA.Chama cha Social Democratic chashinda uchaguzi nchini Austria

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6q

Chama cha Social Democratic Kimeshinda katika uchaguzi wa nchini Austria kinyume na utabiri wa hapo awali.

Chama hicho kilipata asilimia 35.7 ya kura na kuweza kukiacha nyuma chama cha kihafidhina cha kansela Wolfgang Schüssel kilichokuwa kinatawala katika serikali ya mseto.

Wadadisi wanasema pana uwezekano mkubwa wa kuundwa serikali ya mseto baina ya vyama viwili vikubwa na kukiweka kando chama cha mrengo wa kulia kinacho ongozwa na Jörg Haider.